0
Bei ya nyama katika mji wa Mtwara imepanda ghafla toka shilingi 6,000 hadi 8,000 kwa kilo ya nyama mchanganyiko, na steki toka shilingi 7,000 hadi 10,000, bei inayolalamikiwa na wakazi wengi wa mji huo.
Wakizungumza na wanahabari  baadhi ya wakazi hao wamedai wamestushwa kupanda kwa bei ya nyama bila kuelezwa sababu, hali inayowafanya washindwe bei hiyo kuimudu, wakati ikielezwa Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye mifugo mingi wakiwemo ngombe barani Afrika lakini bei kwa mlaji imekuwa ikipanda, na hivyo kuiomba serikali kutafuta namna ya kudhibiti upandaji holela wa bei, sio tu kwa bidhaa hiyo ya nyama, bali na bidhaa zingine, ili kumpunguzia mwananchi ukali wa maisha.

Post a Comment

 
Top