Klabu ya soka ya Simba inayonolewa na kocha muingereza Dylan Kerr huku msaidizi wake akiwa Selemani Matola
imezidi kuingia katika headlines baada ya zile tetesi za muda mrefu
kuthibitika rasmi usiku wa November 11, awali kulikuwa na stori za
mahusiano yasio mazuri kati ya kocha mkuu wa timu hiyo Dylan Kerr na msaidizi wake Selemani Matola.
Kulikuwa na tetesi nyingi kuhusu
mahusiano ya kocha huyo na msaidizi wake kwani inadaiwa iliwahi kufikia
hata kutoaminiana wakati mwingine Kerr alikuwa akizungumza na wachezaji wake Matola alikuwa anatakiwa kutoka nje ila hizo zilikuwa stori tu ila maamuzi ya Selemani Matola kuacha kazi ya kuwa msaidizi wa Kerr yamezidi kuthitibika kuwa yote yaliokuwa yanaandikwa ni kweli.
“Ni
jambo la muda mrefu, huyu kocha hasikilizi ushauri wangu, imefikia sasa
ananichukia na kazi haziendi tena. Sasa nimeona ili kuepusha matatizo
zaidi, nimuachie yeye timu. Nimekutana na uongozi, nimewaambia juu ya
uamuzi wangu, wakanisihi sana nisifanye hivyo, lakini nikashikilia
msimamo wangu. Wakaniambia hata nirudi kufanya kazi timu za vijana,
lakini nikawaambia nitajifikiria kwanza” >>>> Selemani Matola
Selemani Matola aliwahi kuicheza Simba kwa miaka kadhaa na baadae kuwa kocha wa timu ya vijana ya klabu hiyo, lakini Matola aliwahi kucheza Kagera Stars kabla ya kuhamia Simba na mwaka 2005 alitimkia Afrika Kusini kucheza soka la kulipwa katika klabu ya Super Sport United.
CHANZO CHA STORI HII : BIN ZUBEIRY SPORTS- ONL
Post a Comment