0
Siku moja kabla ya kuchezwa kwa mechi ya kimataifa kati ya Taifa Stars dhidi ya Malawi, shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF lilitoa nafasi kwa makocha wa timu zote mbili kuzungumzia mchezo pamoja na maandalizi kuelekea mechi hiyo
Kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Charles Boniface Mkwasa amethibitisha wachezaji wake kuwa katika hali nzuri kuelekea mchezo huo, lakini amekubali kuzungumzia mkataba wake mpya aliyopewa na TFF licha ya kuwa lengo lilikuwa ni kuzungumzia mchezo dhidi ya Malawi.
a (1)
Mkwasa akithibitisha mpango wa kuingia mkataba wa kuendelea kuifundisha Taifa Stars
Mkwasa ambaye alikiri kuingia mkataba na shirikisho la mpira wa miguu Tanzania ili kuendelea kukinoa kikosi cha Taifa Stars, amekiri kufurahishwa na mpango huo, hata hivyo kwa niaba ya TFF afisa habari wake Baraka Kizuguto alithibitisha kuwa Mkwasa amepewa mkataba mpya toka October 1 na atakuwa akilipwa mshahara kama aliyokuwa akilipwa muholanzi Mart Nooij.
a (2)
Baraka Kizuguto akiongea na vyombo vya habari
Ikumbukwe kuwa Mkwasa ni kocha msaidizi wa klabu ya Dar Es Salaam Young African na aliombwa na TFF kuifundisha timu ya taifa ya Tanzania kwa muda wa miezi mitatu ila baada ya kupewa mkataba wa kudumu, Mkwasa ambaye mkataba wake na Yanga unamalizika December 2015 amekiri kuwa atajikita zaidi katika kuifundisha Taifa Stars.

Post a Comment

 
Top