Mshambuliaji wa
klabu ya Manchester City Sergio Aguero anatarajiwa kukaa nje kwa mwezi
mmoja baada ya kupata jeraha nyuma ya goti lake wakati alipokuwa
akiichezea Argentina.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27,ambaye
alifunga mabao matano pekee katika ushindi wa klabu ya City dhidi ya
Newcastle wikiendi iliopita ,alicheza kwa dakika 22 pekee wakati timu
Argentina iliposhindwa na Ecuador.''Nadhani nitakuwa nje kwa kipindi cha mwezi mmoja'' ,Aguero aliiambia TYC Sport katika mji mkuu wa Bueno Aires.
Matatizo ya City vilevile yaliongezeka baada ya David Silva kutoka katika mechi ya ushindi wa 4-0 dhidi ya Luxembourg baada ya kuteguka kifundo cha mguu.
Post a Comment