Klabu ya Sunderland nchini Uingereza imemteua Sam Allardyce kama mkufunzi wa timu hiyo kwa kipindi cha miaka miwili.
Dick Advocaate alijiuzulu kama kocha wa klabu hiyo na kuiwacha ikiwa haijashinda mechi yoyote kati ya mechi nane ilizocheza.Timu hiyo ipo katika nafasi ya pili kutoka mwisho wa jedwali la ligi ya Uingereza.
Allardyce mwenye umri wa miaka 60,amekuwa nje ya ukufunzi tangu alipoondoka katika klabu ya West Ham msimu uliopita.
''Ni Kweli ni kazi yenye changamoto.Lakini nina matumaini kwamba nitaisaidia kuleta uthabiti na mafanikio ambayo kila mmoja anahitaji'',alisema Allardyce.
''Ninajianda kufanya kazi na wachezaji na nitahitaji sana usaidizi wa mashabiki wa Sunderland''.
Allardayce aliwahi kuichezea Sunderland kama mchezaji kati ya mwaka 1980 na 1981 na anakuwa mkufunzi wa kwanza kuwahi kuifunza Sunderland na wapinzani wao Newcastle.
Post a Comment