0


Mchezo umemalizika kwa klabu ya Dar Es Salaam Young Africans kuibuka na ushindi wa jumla ya goli 2-0 dhidi ya watani wao wa jadi Simba, magoli ya Yanga yalifungwa na Amissi Tambwe dakika ya 44 kipindi cha kwanza baada ya kupokea basi nzuri kutoka kwa Malimi Busungu na kuandika goli la kwanza.

 Goli la pili lilifungwa na Malimi Busungu kwa shuti kali lililomshinda golikipa wa Simba Peter Manyika na kuingia wavuni dakika ya 79. Mechi ilimalizika kwa Mbuyu Twite kupewa kadi nyekundu baada ya kuchelewesha muda ukizingatia alikuwa na kadi ya manjano awali.

 Matokeo ya mechi nyingine za Ligi Kuu Tanzania Bara zilizochezwa September 26
  • Coastal Union 0 – 0 Mwadui FC
  • Tanzania Prisons 1 – 0 Mgambo Shooting
  • JKT Ruvu 0 – 1 Stand United
  • Mtibwa Sugar 1 – 0 Maji Maji FC 
  • Kagera Sugar 0 – 0 Toto Africans

Post a Comment

 
Top