1.DIRA-Kuwa na dira ni kujua
unapoelekea na kuwa tayari una picha halisi ya maendeleo yako kichwani.Dira
inatakiwa kiwe kitu ambacho kinawezekana kukamilishwa na kila mmoja kwenye
kundi.
Kiongozi:unaweza ukaona wazo la dira yako
likitekelezeka ,unaweza kuwasilisha dira na malengo yako kwa hatua rahisi na
ndogondogo kwa wanakikundi wenzako wakakuelewa.
Mfuasi:unahitaji kuelewa na
kukubaliana na dira ya kikundi na pia kuelewa kazi zinazohitajika kufanyira na
malengo hakuwezi wa ili kufanyikisha hilo.Pale kila mmoja atakapoweza kuelezea
dira kwa namna moja ,ndipo inakuwa dira ya pamoja ,hii itakupa motisha na
kuongoza vitendo vyenu.
2.kujituma
na kujitoa-kufikia
na malengo hakuwezi kuja kwa kasi kama kumba na kufungua macho,la hasha
,inahusisha kazi kubwa na ya muda
mrefu.kujituma na kujitoa kuna maanisha kutoa muda ,nguvu na ujuzi wako kufikia
malengo.
Kiongozi:ni lazima ujitume na kujitoa kw amalengo yako,wafuasi wako
wanajituma zaidi na kufanya kazi yenye matokeo bora ukiongoza kwa
mfano,kiongozi mzuri anafanya kuhudumia wafuasi wake na si kwa faida yake
binafsi.
Mfuasi:unatakiwa ujitoe kama kiongozi anavyojitoa ,umejipanga na
kujiandaa kutoa mawazo na muda wako
kusaidia kundi zima kufikia dira yenu.
3:Kujiamini:ni
kuwa na imani kwamba kitu kiko sahihi na uamuzi uliofanywa ndiyo sahihi
na bora zaidi,kuamini kwamba anaweza kutenda kazi yake kwa ufanisi.Ili kuweka
mwelekeo,kiongozi anahitaji kuonekana uwezo wake akiwa ametulia katika nafasi yake
.Hii inawahamasisha WENGINE
KUJIAMINI na kutoa msaada wa kuhakikisha kiongozi anafanyikiwa .
Kiongozi:Ili kuweka mwelekeo ,kiongozi unahitaji kuonekana unajiamini
kuhusu uwezo wako na unaiweza nafasi yako unatakiwa uwe na unyenyekevu wa
kusikiliza maoni ya wengine,kukiri unapokosea na kutambua hekima ya wengine.
Mfuasi:unatakiwa uwe na imani na kiongozi na uelewe kwamba wote mnafanya
kazi kuelekea lengo mojdilifua lakini uaminifu wako usiwe bila kipimo
,unatakiwa ujiamini kiasi cha kusimama
na kuzungumza pale unapoona kiongozi amekosea au unapoona kunafanyika
kitu kinyume cha maadili.
4;Mawasiliano-kitu cha muhimu kujua kuhuisu mawasiliano ni kwamba huo ni mchakato wa njia
mbili,kusikiliza ni muhimu kama ilivyo muhimu kuzungumza. Kuwafanyawatu wote
wafanye kazi pamoja unahitaji kushirikisha wengine juu ya dira na malengo kwa
uwazi na kueleza kile ambacho kinahitajika kufanyika. Mawasiliano mazuri
yanasaidia kila mmoja kujifunza kutokana na makosa na kuweza kwenda mbele.
Kiongozi:Unahitaji kutoa taarifa kuhusu uamuzi
na kutoa mwongozo na kueleza vizuri juu ya ubnachotaka
kifanyike.Unahitajikuwapa moyo na msaada wanaokuzunguka .
Mfuasi;Unaweza kuzungumza na kiongozi na
wafuasi wengine. Viongozi wanahitaji mtu
wa kuwaambia mambo yanayokwenda vizuri na yale yanayokwenda kombo,ili waweze
kufanya uamuzi bora.
5.Uadilifu:Uadilifu maana yake ni kufuata kanuni za maadili. Uaminifu ni sehemu
muhimu ya uadilifu na ukiwa mwadilifu unaweza kuaminiwa kw a sababu kamwe hutaliweza kukiuka
maadili na hata wakati ambao yanaweza kuwanufaisha wenyewe. Kwa mfano, mtu
mwadilifu hawezi kuchukuwa rushwa.
Kiongozi:Ni mkweli na muwazi kwa wafuasi
wake. Utaaminika kwa sababu unatenda unachosema.lazima pia uwe mwangalifu na
mahitaj ya watu wengine.mamlaka ya kweli huzaliwa kutokana na heshima,tabia
njema na uaminifu kwa kila mtu ambaye unamuongoza.
Mfuasi.. Kiongozi
anahitaji kukuamini kwamba unafanya kile unachotakiwa kufanya, anakuaminia.
Uadilifu huendeleza tabia na hujenga uwajibikaji ,uwazi na uaminifu. Hii ni
misingi ya kukujenge heshima kutoka kwa wale walio karibu yako au unaowaongoza
, ikiwa ni pamoja na wanafunzi wenzanko, wanatimu wenzanko au hata wapiga kura
wako.
6. Uwajibikaji : uwajibikaji ni kuwa mkweli kwa wale
unaowawakilisha. Pia ni wajibu wa kila mmoja, viongoz na wafuasi,kuhifadhi na kuripoti
shuguli zao, kukubali wajibu wao na kutoa matokeo katika njia ya uwazi. Hii
vilevile, inahusisha wajibu wa matumizi ya fedha au mali nyingine.
Kiongozii: unawajibika na unatakiwa ujitahidi kupata matokeo bora kutokana na
utendaji wako, pia kuchukua hatua zaki uwajibikaji pale kundi zima
linaposhindwa kutimiza wajibu bila kujali makosa gani yamefanyika.
Mfuasi: unatakiwa
kuchukua umiliki kamili wa majukumu yako na uwasaidie wenzako’ ukijua kuwa
mafanikio ya kundi hayawezi kuzidi yale ya mmoja wao alie mtendaji dhaifu
kuliko wote!
WATU WENGI SI VIONGOZI WAZURI NA WENGINE WALA HAWATAKIWI
KABISA KUWA VIONGOZI ,ILA WANAWEZA KUWA WAFUASI WAZURI VIONGOZI BORA WANAITAJI
WAFUASI BORA
Post a Comment