0

Mkazi mmoja aliyejulika kwa jina la Kesi Mkwinda amegongwa na gari aina ya kenta na kufariki dunia hapo hapo majira ya saa 9:45 jioni ya leo katika kitongoji cha Mapambano kijiji cha Nduruka kata ya Mbaya wilaya ya Liwale mkoani Lindi.

Mtendaji wa kijiji hicho cha Nduruka bwana Hamidu Kimbunga alithibitisha kutokea kwa tukio hilo nae OCD wa Liwale Raphael Yohana amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Shuhuda wa tukio hilo Juma Pyale alisema Kesi Mkwinda alikuwa emesimama nyuma ya bodi ya gari huku akiongea na watu waliokuwa ndani ya gari Mara dereva aliyekuwa anaendesha alirudisha gari nyuma na kumgonga na kumkanyaga na kupelekea kupoteza uhai.

Baada ya kutokea tukio hilo dereva Alitoweka na gari kuelekea Liwale mjini kufika mbele baada ya kumaliza majuma ya kijiji cha Nduruka alisimama na kuliacha gari na kutimua mbio kusikojulikana na jina la dereva halikupatina lakini gari limekamatwa na polisi.

Hapa chini ni wananchi waliokuwa eneo la tukio katika kijiji cha Nduruka.

Post a Comment

 
Top