0

Mgombea mwenza wa Urais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania,Samia Suluhu kupitia Chama cha mapinduzi ccm amefanya  mkutano wa kujinadi kukipigia chama chake kura na kuwanadi wagombea wa Udiwani na Ubunge wa jimbo la Liwale, Faith Mitambo mkutano uliofanyika leo katika uwanja wa Nanjinji uliopo kata ya Likongowele Liwale mjini.

Katika mkutano huo mbunge wa Jimbo la Liwale alianisha kero 8 zinazowakumba wananchi wa jimbo hilo ambazo hazijapatiwa ufumbuzi wa kudumu miongoni mwa  kero hizo ni kukosa Soko la korosho,Barabara,Elimu,Afya,Maji,Mawasiliano,Umeme na Migogoro ya ardhi.

Samia Suluhu alisema kama wananchi watakipigia kura za ndio chama cha mapinduzi serikali yake wataweza kutatua changamoto hizo zinazowasumbua wananchi wa jimbo la Liwale kwa wakati ikiwemo kero ya kukosa kupata pembejeo za kilimo akiwa madarakani atawaletea pembejeo kwa wakati na ataimalisha vyama vya ushirika.

Suala la Afya pia alisema serikali yake itaboresha huduma ya afya kwa kuwaleta watumishi na vifaa tiba kwa kila kituo cha afya,,mawasiliano kila kijiji kutajengwa minara ya simu,umeme mpango wa kusambaza umeme vijijini REA umeanza kwenda baadhi ya vijijini,Migogoro wa ardhi serikali yake itakuwa na mpango wa kupima upya mipaka yote ambayo yenye migogoro. 

PIA SAMIA AWATAKA WANALIWALE KUSOMESHA WATOTO

Mgombea mwenza Samia Suluhu Hasani akiwa na mgombea ubunge jimbo la Liwale Faith Mitambo wakati alipokuwa wilayani kwenye ziara ya kuomba kura 


  Mwenyekiti wa kmatai ya ulizi na usalama LIWALE MR MMBAGA  wakwanza kushoto akiwa kwenye  mkutanoa wa mgombea mwenza Samia Suluhu
Wazazi na walezi wilaya Liwale mkoa Lindi wametakiwa kuwasomesha watoto wao ili waweze kukabiliana  na  upungufu wa watumishi unaoikabili wilaya hiyo.

Wito huyo umetolewa na mgombea mwenza wa chama cha mapinduzi Samia Suluhu wakati alipokuwa anazungumza na wananchi wa wilaya hiyo kwenye mkutano wa kampeni wa kuomba kura kwa wananchi kuwa chagua  viongozi wa chama cha mapinduzi.
Samia alisema kuwa yeye kama mama anaumia sana  anapo waona watoto wanaostaili kwenda  shule wanazurura mtaani hivyo basi wazazi na walezi ni wajibu wa kuwapelekea wato to shule kwani hata vitabu vya  dini vinaagiza kusomesha watoto.
 Alisema kuwa wazazi na walezi wasipowapeleka watoto  wao shule wataendelea kulalamikia kuwa kuna upungufu wa watendaji katika idara za serikali  kumbe imesababishwa  na wazazi  kutotilia maana elimu ya watoto wao.
Alisema  chama cha mapinduzi kwa kutambua umuhimu wa elimu katika ilani yake ya uchaguzi imesema itasomesha watoto bure kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha sita hivyo ni vyema muda utakaofika wa kupiga kura wakaipigia chama hicho ili kiweze kutekeleza na kutimiza ahadi hiyo.
 mgombea ubunge wa jimbo hilo Faith Mitambo alisema wilaya ya Liwale inakabiliwa na changamoto  nyingi ikiwemo , mawasiliano,kukosa soko la uhakika la mazao ya biashara, ufut  na korosho pamoja na mahusiano mabaya kati ya idara ya selous na wananchi wanaoishi mipakani mwa hifadhi hiyo hali ambayo inasababisha wananchi wanaoingia katika hifadhi hiyo kupoteza maisha kwa njia ya utatanishi.


Post a Comment

 
Top