ANUANI YETU Email:2015mvili@gmail.com
KATIBA YA MTANDAO WA VIJANA LIWALE-(MVILI)
LIWALE YOUTH NETWORK-(LIYONE)
UTANGULIZI
DIRA YETU
DHIMA YETU
IBARA YA I
1.0: SEHEMU YA
I JINA
1.2: ANAUANI NA
MAHALI
1.3: ASILI
IBARA YA II
2.0: MALENGO YA MVILI/LIYONE
IBARA YA III
2.2: MAMLAKA
IBARA YA IV
3.0:
UANACHAMA (MVILI/LIYONE).
3.2.0: HADHI YA
MWANACHAMA
3.3.0: UKOMO WA MWANACHAMA
3.4.0: HAKI NA WAJIBU WA MWANACHAMA
IBARA YA V
4.1.0:
UONGOZI WA KIKUNDI/ASASI
4.1.1:KAMATI
TENDAJI
IBARA YA VI
5.0: MAJUKUMU YA VIONGOZI WA KIKUNDI/ASASI
5.1.0: MWENYEKITI MTENDAJI
5.1.1:
MAKAMU MWENYEKITI MTENDAJI
5.2.0:
KATIBU MKUU MTENDAJI
5.3.0: MWEKA HAZINA
6.O: MKUTANO
MKUU
6.2.0: SHUGHULI
ZA MKUTANO MKUU.
6.3.0: MKUTANO MKUU MAALUM
7.0: CHOMBO CHA
USHAURI (UBALOZI)
8.0: MASWALA YA
FEDHA
9.0:
MABADILIKO YA KATIBA YA MTANDAO WA VIJANA LIWALE
9.2.0: KUVUNJWA KWA KIKUNDI.
i
KATIBA YA MTANDAO WA VIJANA LIWALE-(MVILI)
LIWALE YOUTH NETWORK-(LIYONE)
ASASI ISIYO YA KISERIKALI NA ISIYO YA KUPATA FAIDA
UTANGULIZI
Vijana ndiyo kundi rika kubwa katika jamii yetu ya
sasa ya Liwale na hata taifa kwa ujumla.Uwepo wa wingi huo wa vijana unatoa uhakikisho wa uwepo wa nguvu
kazi na nguvu fikra za kutosha ambazo ni hitaji muhimu sana kwa Maendeleo
endelevu ya jamii yetu ya sasa na ya baadae.
Hata hivyo nguvu kazi na nguvu fikra hizo za vijana,
ili ziwe na tija stahiki na tarajiwa kwa jamii ni sharti ziendelezwe kwenye
uwelekeo chanya.
̎Hakuna kesho nzuri ya Liwale
kama vijana watapuuzwa - ̎ waasisi.
Hivyo kwa
kuzingatia, vijana wa Liwale wamegawanyika katika makundi mbalimbali
yasiyoungana na yasiyoshirikiana kwa hiyo
ni nadra kuleta tija itarajiwayo katika jamii na;
Kwa kuwa, mazingira yetu ya sasa
tuliyomo yanakosekana jukwaa unganishi
ambalo kama vijana tungeweza kuchangia mawazo,fikra,changamoto,
uzoefu na kubadilishana ujuzi kwa Maendeleo yetu na
Maendeleo ya jamii yetu kwa ujumla.
Hivyo basi tumeshawishika kuanzisha Mtandao wa
Vijana utakaolenga
kuunganisha vijana na kuziba kabisa ombwe linalofifisha jitihada za vijana kuwa
na tija stahiki kwa jamii.
DIRA YETU
Kuwa na Liwale iliyostawi yenye kizazi cha
vijana wenye uelewa na uthubutu mpana wa kushiriki kwenye shughuli mbalimbali
za kiuchumi,kijamii na kiutamaduni kwa maendelo endelevu ya jamii nzima kufikia
2035.
DHIMA YETU
Kuwawezesha
vijana ili waweze kuwa na njia au
mbinu bora kabisa za kushiriki na kuendeleza,fikra, mawazo,vipaji,uelewa na
uthubutu kwenye masuala mbalimbali ya kiuchumi na kijamii kwa manufaa yao
wenyewe na ya jamii kwa
ujumla.
KAULI MBIU
“Fikra mpya matumaini mapya ishi mabadiliko”
ii
IBARA YA I
1.0: SEHEMU YA
I JINA
1.1: Jina la asasi litakuwa ni;
MTANDAO WA VIJANA LIWALE ( MVILI)
1.1: (a) Bila ya kuathiri matumizi ya jina hilo,tafsiri ya kiingereza ya
jina hilo yaweza kutumika sambamba, nayo ni;
LIWALE YOUTH NETWORK (LIYONE)
1.2: ANAUANI NA MAHALI
Makao makuu ya (MVILI/LIYONE)
yatakuwa wilayani Liwale kujumuisha jengo la ofisi,anuani za posta,barua pepe
na aina nyingine yeyote ya Mawasiliano.
1.3: ASILI
Ni asasi isiyo ya kiserikali na
isiyo ya kupata faida na haifungamani
na chama chochote cha siasa
IBARA YA II
2.0: MALENGO YA MVILI/LIYONE
2.1: Malengo ya (MVILI/LIYONE) yatakuwa ;
i.
Kuunganisha vijana walio ndani na nje ya Liwale
katika kuchochea
Mabadiliko kuelekeza kuyafikia maendeleo ya vijana na jamii kwa ujumla.
ii.
Kuhamasisha na kujenga uelewa mpana kwa vijana
kuwa wazalendo,
waadilifu na moyo wa kujitolea kwa ajili ya maendeleo na jamii kwa
ujumla.
iii.
Kuhamasisha na kuanzisha kampeni mbalimbali za
kujenga
uelewa kama Elimu,Afya,Mazingira
na masuala mengine mtambuka.
iv.
Kujenga uelewa kwa jamii dhidi ya VVU na UKIMWI
v.
Kuwa
sauti ya vijana/kupaza sauti za vijana
katika kuelezea changamoto zao
mbalimbali za kimaisha.
vi.
Kuhamasisha uelewa na umuhimu wa kutunza
mazingira .
vii.
Kuhamasisha michezo,burudani na utamaduni
katika jamii yetu.
viii.
Kuandaa
na kuendesha semina za kujenga uelewa
katika
masuala ya kisheria,biashara na ujasiriamali.
1
IBARA YA III
2.2:
MAMLAKA
Ili kufikia malengo
yaliyowekwa kwa mujibu wa katiba hii na si vinginenvyo, kikundi/asasi kupitia
kamati tendaji yake inaweza kutekeleza yafuatayo;
i.
kuajiri vibarua au wafanyakazi wa kudumu
ii.
Kukodisha
au kumiliki majengo
iii.
Kufungua
akaunti benki
iv.
Kuanzisha
na kuratibu semina,warsha na matukio mbalimbali ili kujenga
uelewa kwa vijana na jamii kwa ujumla
v.
Kufanya kazi za mashirika,asasi na vyombo vya
kiserikali kwa kubadilishana
taarifa.
vi.
Kutunisha mfuko wa kikundi/asasi kwa kutumia
harambee
vii.
Kupanga
kiwango cha ada ya uanachama na michango mingine.
viii.
Kufanya chochote ambacho hakivunji katiba na
sheria za nchi kwa lengo la
kutunza
mali za kikundi/asasi.
IBARA YA IV
3.0: UANACHAMA (MVILI/LIYONE).
3.1.0: Uanachama wa Mtandao wa Vijana uko wazi
kwa mtu yeyote atakayetimiza vigezo vifuatavyo;
i.
Awe na umri kuanzia miaka 18 na kuendelea.
ii.
Kuwa tayari kulipa ada ya uanachama na michango
mingine.
iii.
Kufuata na kutii kanuni,taratibu na miongozo
mbalimbali ya kikundi.
iv.
Awe na akili timamu.
v.
Awe na tabia njema katika jamii
vi.
Awe muadilifu
vii.
Awe na mtazamo chanya wa kuleta mabadiliko ya
kujenga taifa .
2
3.1.1: Bila kuathiri masharti
yaliyowekwa (3.1.0 kuanzia kifungu kidogo cha( i – vii) shirika au asasi iliyo
ndani au nje ya wilaya inaweza kuwa mwanacha
iwapo malengo yake yanafanana na (MVILI/LIYONE).
3.1.2: Bila kuathiri Masharti
yaliyowekwa (3.1.0) Mtu yeyote anaweza kuwa mwanachama wa kikundi bila kujali jinsi,rangi,dini wala aina nyingine
yeyote ya ubaguzi.
3.2.0: HADHI YA MWANACHAMA
3.2.1: Kila mwanachama au
shirika/asasi ndani ya kikundi watakuwa na hadhi sawa na kila mmoja atakuwa na
kura moja kwenye mkutano mkuu.
3.2.2: Kila shirika/asasi au
mwanchama watateua mwakilishi kushiriki kwenye mikutano ya kukundi kwa
kutaarifu jina la mwakilishi husika kwa katibu wa kikundi.
3.3.0: UKOMO WA MWANACHAMA
3.3.1: Uanachama wa mwanchama
yeyote unaweza ukatenguliwa na kamati tendaji ya kikundi kwa nia njema lakini
mwanchama atakuwa na haki ya kusikilizana na kamati tendaji kabla ya uamuzi wa
mwisho kufikiwa juu ya hatma ya uanachama wake.
3.3.2: Mwanachama kwa hiari yake
anaweza kujiuzuru uanachama kwa kuuharifu uongozi wa kamati tendaji kwa maandishi.
3.3.3: Mwanachama atakaejiuzuru ama kufukuzwa kwenye kikundi hapatakuwa na
urejeshaji wa aiana yeyote ya fidia kwa nguvu au mchango uliyotolewa na
mwanachama huyo.
3.4.0: HAKI NA WAJIBU WA MWANACHAMA
i.
Kuhudhuria mkutano na kufanya maamuzi kwa kupiga
kura.
ii.
Kulipa
ada na michango mingine kama itakavyopangwa.
iii.
Kuwa na
haki ya kuchagua na kuchaguliwa.
iv.
Kuwa
mlinzi wa mali ya chama.
v.
Kutetea,kusambaza taarifa mbalimbali za kikundi daima.
vi.
Kuonyesha
tabia njema na maadili mazuri wakati wote.
3
IBARA YA V
4.1.0: UONGOZI WA KIKUNDI/ASASI
4.1.1: Kikundi/asasi itaongozwa na
vyombo viwili vya kimaamuzi ambavyo ni mkutano mkuu na kamati tendaji pamoja na
chombo kimoja cha ushauri kitakachojulikana kama balozi.
4.1.1:KAMATI TENDAJI
4.1.2: Kamati tendaji itaundwa na
watu wasiozidi nane (8) kati yao wataingia kwenye kamati kwa kofia za vyeo vyao
nao ni Mwenyekiti mtendaji,Katibu mtendaji na Mweka hazina. Wajumbe wengine
wanaosalia watachaguliwa kwenye mkutano mkuu wa kikundi.
4.1.3: Kamati tendaji itakua
inakutana angalau mara moja(1) kila mwezi.
4.1.4: Mwenyekiti mtendaji atakua
muongozaji wa vikao vyote vya kamati tendaji na kolamu ya vikao vyote vya
kamati kuu tendaji itakuwa robo tatu ya idadi ya wajumbe.
4.1.5: Upigaji kura wa kwenye
vikao vyote vya kamati tendaji itafanywa kwa kunyosha kidole au kura ya siri.
4.1.6: Ikitokea kura zimefungana
Mwenyekiti atakua na KURA YA ZIADA.
4.2.0: Kama ikitokea mjumbe mmoja
wa kamati tendaji ameenda kinyume na matakwa ya katiba hii kamati tendaji inaweza kwa wingi wa idadi ya kura usiopungua
robo tatu (3/4) inaweza
kumuondoa mjumbe yeyote wa kamati tendaji madarakani huku ikizingatiwa
kwamba mtu huyo amepewa haki ya kusikilizwa kabla ya uamuzi wa mwisho.
4.2.1: Kamati tendaji
inaweza ikamteua mtu mwingine kuwa mjumbe wa kamati tendaji kuziba nafasi
iliyoachwa wazi, ikizingatiwa robo tatu (3/4) ya kura zilizopigwa zimependekeza
jina moja.
4
IBARA YA VI
5.0: MAJUKUMU YA VIONGOZI WA KIKUNDI/ASASI
5.1.0: MWENYEKITI MTENDAJI
i.
Kuilinda na kuitetea katiba ya kikundi/asasi kwa
juhudi zake,maarifa yake yote na nguvu zake.
ii.
Kuwa mwenyekiti wa vikao vyote vya kamati
tendaji na mkutano mkuu wa kikundi/asasi
iii.
Kuongoza na kusimamia kazi za kazi za kikundi
kwa mifano ya kuigwa.
iv.
Kuandaa na kutoa taarifa za kikundi kwenye
mkutano mkuu.
v.
Kuwa mweka sahihi wa nyaraka zote za kikundi
pamoja na akaunti na miamala yote ya kifedha inayofanywa na kikundi.
vi.
Kuwa msemaji na mtetezi mkuu wa kikundi.
vii.
Kuliwakilisha
kundi kwenye mikutano,shughuli na dhifa mbalimbali ambazo kikundi
kitakua kinaalikwa.
5.1.1:
MAKAMU MWENYEKITI MTENDAJI
i.
Kumsaidia Mwenyekiti mtendaji na kusimamia
shuguli na majukumu kama yalivyoelekezwa kwa mujibibu wa katiba(ibara ya v kifungu cha 5.1.0 kifungu kidogo i – vii) endapo Mwenyekti mtendaji
hayupo.
ii.
Kutekeleza majukumu mengine kama yatakavyopangwa
na Kamati tendaji.
5.2.0:
KATIBU MKUU MTENDAJI
i.
Kuitisha vikao vyote halali vya kikundi/asasi
kwa kushirikiana na Mwenyekiti mtendaji.
ii.
Kuwa katibu wa vikao vyote halali vya
kikundi/asasi.
iii.
Kupanga,kuendeleza na kusimamia shughuli za kila
siku za kikundi/asasi .
iv.
Kuandika na kutunza kumbukumbu,mihutasari
mbalimbali ya vikao na mikutano ya kikundi/asasi .
v.
Kukusanya na kusambaza taarifa mbalimbali ndani
ya kikundi.
vi.
Kutunza na kusimamia mali zote halali za
kikundi/asasi.
vii.
Kufanya shughuli zingine zozote ambazo ni halali
na zitalinda maslahi ya kikundi/asasi kama itakavyopaswa au kuamuliwa na kamati
tendaji.
5
5.3.0: MWEKA HAZINA
i.
Kubuni mbinu za kongeza mapato ya kikundi/asasi.
ii.
Kuandaa,kutoa na kuweka kumbukumbu sahihi ya
taarifa ya mapato na matumizi ya kikundi/asasi.
iii.
Kutunza nyaraka zote halali za mahesabu za
kikundi/asasi .
iv.
Kupokea michango na ada za uanachama wa kikundi.
v.
Kufanya malipo yote halali ya kikundi/asasi .
vi.
Kuwa mweka sahihi wa nyaraka zote za kikundi
pamoja na akaunti na miamala yote ya kifedha inayofanywa na kikundi.
vii.
Kufanya shughuli
au majukumu yote halali ya kifedha kama yatakavyoelekezwa au kuamuliwa
na kamati tendaji.
6.O: MKUTANO MKUU
6.1.0: Kutakuwa na mkutano mkuu ambao utafanyika
mwezi wa 12 kila mwaka, tarehe ya mkutano itapangwa na kamati tendaji.
Wajumbe wa Mkutano Mkuu ni
Wanachama wote halali na hai wa kikundi/asasi lakini pia kuna uwezekano wa
kuwepo na wageni waalikwa kama kamati tendaji itaridhia kuwaalika.
6.1.1: Wanachama wote watapewa taarifa juu ya uwepo
wa mkutano mkuu angalau siku 14 kabla ya kufanyika kwa mkutano mkuu.
6.1.2: Akidi ya mkutano mkuu itakuwa angalau
nusu(1/2) ya Wanachama wote.
6.2.0: SHUGHULI ZA MKUTANO MKUU.
i.
Kupokea na kujadili taarifa ya Mwenyekiti
mtendaji kuhusu shughuli za kikundi kwa mwaka nzima.
ii.
Kupokea na kujadili taarifa ya mapato na
matumizi ya kikundi/asasi.
iii.
Kuchagua kamati tendaji ya kikundi/asasi.
iv.
Kujadili jambo lolote kadili litakavyoweza
kuamuliwa.
v.
Kutoa mapendekezo ya kubadili katiba au
kutengeza kanuni za kikundi pale inapobidi.
vi.
Kuchukuwa hatua za kinidhamu dhidi ya viongozi
wa kikundi/asasi waliokiuka katiba hii.
vii.
Kupitisha kanuni na miongozo ya kinidhamu dhidi
ya uvunjifu wa katiba, kanuni na miongozo ya kikundi/asasi
6
6.3.0: MKUTANO MKUU MAALUM
6.3.1: Muda wowote kunaweza
kuitishwa mkutano mkuu maalumna kamati tendaji ya kikundi/asasi au robo ya
wanachama kwa kuiharifu kamati tendaji ya kikundi kujadili jambo la dharula
,katibua atawajulisha wanachama angalau siku 14 kabla ya kufanyika kwa mkutano
mkuu maalum pamoja na ajenda itakayojadiliwa.
7.0: CHOMBO CHA USHAURI (UBALOZI)
Kamati tendaji itaunda chombo cha ushauri kitakachojulikana kama
balozi.
7.1.0: Kutakuwa na balozi
shawishi na balozi unganishi.
7.1.1: Balozi shawishi itaundwa
na wajumbe wazee wasiozidi watatu(3) na kazi yao kubwa nikutoa ushauri
mbalimbali kwenye mipango na shughuli za
kikundi.
7.1.2: Balozi unganishi nazo
zitaundwa na wajumbe vijana si zaidi ya watatu na kazi yao kubwa itakuwa
kuunganisha vijana kwenye maeneo watayowepo
7.1.3: balozi shawishi na balozi
unganishi ndio zitakuwa ndio balozi zetu nje ya makao makuu yetu au nje ya
wilaya.
8.0: MASWALA YA FEDHA
i. 9.0: Pesa yeyote itakayokusanywa na balozi
itatumika kwa malengo ya kikundi.
ii. Akaunti
ya benki itakayofunguliwa itakuwa na jina la kikundi.
iii. Malipo
au miamala yeyote halali lazima lazima iandikwe na kumbukumbu zake zitunzwe.
iv. Watia
sahihi katika akaunti ya kikundi lazima
wawepo jumla wajumbe au wanachama wasiopungua watano (5).
7
9.0: MABADILIKO
YA KATIBA YA MTANDAO WA VIJANA LIWALE
9.1.0:
Katiba inaweza kubadilishwa yote au kifungu kimoja kama zaidi ya
theluthi mbili (2/3) ya wanachama watakubali mapendekezo hayo na kuyapigia kura
ya ndiyo kwenye mkutano mkuu.
9.2.0: KUVUNJWA KWA KIKUNDI.
9.2.1:
Kikundi kinaweza kuvunjwa kama zaidi ya theluthi mbili (2/3) ya
wanachama wataunga mkono maamuzi hayo kwenye mkutano mkuu.
9.2.2: Kama
kikundi kitavunjwa baada ya madeni kulipwa kama yapo,
Mali na Pesa za kikundi zinaweza kuhamishiwa katika
kikundi kingine ambacho kina malengo yanayofanana au ikitokea hakutokuwepo kwa kikundi/asasi
namna hiyo, Mali na Pesa hizo zitatolewa kwenye familia ama watu masikini
wasiojiweza.
8
Post a Comment