Wilaya ya Liwale mkoani Lindi pamoja na mkoa wa Mtwara inahitaji kujengwa viwanda vya kubangulia korosho na kukamulia mafuta ya zao la ufuta ili kuweza kuongeza thamani ya mazao na kuongeza kipata .
Mgombea urais kupitia cha ACT-Wazalendo mama Anna Mghwira aliyasema hayo kwenye mkutano uliofanyika katika uwanja wa Nanjinji uliopo kata ya Likongowele Liwale Mjini leo wakati akiomba ridhaa kwa wananchi ili apigiwe kura ili aweze kuwa rais wa Tanzania.
Mghwira alisema chama chake kimeandaa Sera mzuri na rahi ambazo zinaweza kutekelezeka kwa urahi hivyo amewaomba wananchi kuwapigia kura wagombea wa nafasi za Ubunge na madiwani uliogombea kupitia chama cha ACT-Wazalendo.
Alisema serikali yake itakuwa Uchumi shirikishi kwa lengo la kuwainua wakulima,ataboresha huduma za Afya ambazo sasa imekuwa kero na mzigo mkubwa kwa wananchi kwani hospitali nyingi hakuna dawa na aliongeza kuboresha Elimu ili kumkomboa Tanzania kukosekana haya yote ni kutokana na Tanzania hakuna siasa safi na hakuna uongozi safi.
Mgombea Ubunge jimbo la Liwale kupitia chama cha ACT-Wazalendo, Imani Omari Mtesa alisema kama wananchi watampa ridhaa atahakikisha ataboresha miundo mbinu ya barabara,maji na ataboresha huduma za afya.
Post a Comment