LIWALE-LINDI
TIMU ya soka ya Mmungurumo jana imetinga fainali ya kombe la Mbuzi Cup baada ya kuitungua Masaki FC kwa mabao 3-2 mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Shule ya msingi Muungano Kata ya
Nangando Wilayani Liwale mkoani Lindi.
Mchezo huo ulikuwa ni kuvutia kutokana kila pande kucheza
soka la kuvutia na kutambuana mbinu zao kwa kuwa ni mahasimu wa kubwa
wa mji wa Liwale.
Timu ya Masaki ilikuwa ya kwanza kutikisa nyavu za Mmungurumo na kuandika mabao mawili kwa haraka zaidi lakini hayakudumu sana, ndipo kabla ya kwenda mapumuziko Mmungurumo ilisawazisha mabao yote na kupelekea wanaenda mapumuziko zilikuwa sare ya mabao 2-2.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi na timu zote zilicheza kwa kukamiana lakini Mmungurumo ilifanikiwa kujipatia bao lake la tatu na la ushindi katika dakika za lala salama kabla refa kupuliza kipyena cha mwisho ambapo Mmungurumo ilichomoza na ushindi wa mabao 3-2 ya Masaki FC.
watu kazini wakitifuana katika Ligi ya Mbuzi inayoendelea kwenye Uwanja wa Nangando Wilayani Liwale.
watu kazini wakitifuana katika Ligi ya Mbuzi inayoendelea kwenye Uwanja wa Nangando Wilayani Liwale.

Post a Comment