Na mwaandishi wetu
CHAMA cha wananchi (CUF)
taifa kimekabidhi msaada wa bati 60 pamoja na vifaa mbalimbali vya ujenzi
vyenye thamani ya Sh.milioni 1.2 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa
katika shule ya msingi Mpulima iliyopo katika kata ya Mbuyuni Halmashauri ya
wilaya ya Masasi mkoani hapa.
Akikabidhi msaada huo juzi
kijijini hapo kwa uongozi wa shule hiyo kwa niaba ya mwenyekiti wa Chama hicho
taifa,Prof.Ibrahim,Lipumba,mkurugenzi wa mipango na uchaguzi
taifa,Shaweje Mketo alisema kama kawaida Chama cha CUF kinaendelea kutathamini
na kutatua huduma za msingi wanazozikosa wananchi.
Alisema msaada huo ni
sehemu ya utekelezaji wa ahadi ya mwenyekiti wa Chama hicho taifa Prof.Ibrahim
Lipumba aliyoitoa mapema mwaka huu baada ya kufanya ziara katika shule hiyo na
kukuta hali ya madarasa yakuwa kwenye mazingira magumu na baadhi ya wanafunzi
wakisoma chini miti kwa kukosa vyumba vya madarasa.
Mketo alisema kuwa licha
ya Chama hicho kuwa na uwezo mdogo wa kifedha lakini kinaona upo umuhimu wa
kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi kwakuwa serikali iliyopo madarakani
imeshindwa kuwatatulia changamoto hizo.
Alisema kutokana na
wanafunzi wa shule hiyo kukosa miundombinu rafiki ya vyumba vya madarasa Chama
cha wananchi (CUF) kimeamua kutoa msaada huo wa bati 60 pamoja na vifaa vingine
vya ujenzi ikiwemo misumari vizibo vya kugongea bati.
“Sisi kama Chama cha
wananchi CUF tumeguswa na tatizo hili la shule ya msingi Mpulima ndio maana
tumechukua jukumu la kutoa msaada huu wa bati ili kusaidia ujenzi wa vyumba vya
madarasa ii watoto hawa wasienelee kusomea chiti miti,”alisema Mketo
Alisema Chama hicho
kinataendelea kutoa misaada mbalimbali ya kijamii ili kuhakikisha wananchi
wanaondokana na changamoto zinazowakabili ambazo serikali ya CCM imeshindwa
kuzipatia ufumbuzi kutokana na viongozi wake kutojali matatizo ya wananchi.
Aidha Mketo kwa niaba ya
Chama hicho alitoa fedha sh.150,000 kwa ajili ya mafundi watakaotengeneza
vyumba hivyo vya madarasa ili jitihada hizo za matengenezo zifanyike kwa haraka
hatimaye wanafunzi waweze kusomea madarsa hayo haraka.
Akipokea msaada huo
mwalimu mkuu wa shule hiyo Semeni Nyumayo alikipongeza Chama hicho kwa
kutoa msaada huo wa bati na kueleza kuwa awali wanafunzi wake
walikuwa wakisomea chiti ya miti kutokana na ukosefu wa vyumba vya madarasa.
Alisema shule hiyo ina
jumla ya wanafunzi 599 wa kuanzia darasa la kwanza hadi la saba na kwamba kwa
muda mrefu wanafunzi wa darasa la sita walikuwa hawana chumba cha darasa na
kuanzia sasa vyumba hivyo viwili vitakamilika na wanafunzi hao wataondokana na
adha hiyo ya vyumba vya madarasa.
Post a Comment