Shirikisho
la Mpira wa Miguu nchini Tanzania (TFF) imekubali kuwa wenyeji wa
michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati ngazi ya vilabu
inayojulikana kama Kagame Cup.
Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu
Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) ambao ndio wamiliki wa mashindano haya
na hutoa mialiko kwa vilabu vyenye sifa ya kushiriki. Watatoa orodha ya
vilabu shiriki na ratiba ya michuano hiyo baade mwezi huu au mapema
mwezi ujao.Afisa habari wa TFF, Baraka Kizuguto amesema uamuzi wa kukubali kuwa wenyeji umetolewa na shirikisho hilo mapema Jumapili baada ya kuombwa na Cecafa.
Michuano hii inatarajiwa kufanyika nchini Tanzania kuanzia tarehe 11 Julai mpaka 02 Agosti 2015.
Michuano hiyo inadhaminiwa na Raisi wa Rwanda, Paul Kagame na hufanyika kila mwaka katika nchi mwanachama za ukanda wa Afrika ya Mashariki na Kati. Rwanda ndio ilikuwa mwenyeji wa michuano ya mwaka jana inayohusisha vilabu.
Post a Comment