Mshambuliaji
wa klabu ya Yanga Simon Msuva amerejea nchini Tanzania akitokea nchini
Afrika ya Kusini alipokwenda kufanya majaribio kwa ajili ya kucheza soka
la kulipwa.
Msuva aliripotiwa kutoroka kuelekea nchini humo kufanya majaribio katika klabu inayoshiriki ligi kuu ya Bidvest Wits.Msuva, ambaye ameiwezesha Yanga kuwa mabingwa akiwa mfungaji bora baada ya kupashika mabao 17, ameiomba Yanga kumkubalia kujiunga na timu hiyo endapo atafuzu jaribio lake baada ya kurejea kwake siku Jumapili.
Habari zinasema kuwa mabosi wa Bidvest wameridhishwa na mchezaji huyo na wanafungua milango ya mazungumzo na timu yake ya Yanga ili kumsajili kwa gharama yoyote.
Msuva alijiunga na Yanga mwaka 2012 akitokea timu ya Moro United na amefunga magoli 35 katika mechi 102 alizoichezea Yanga katika michuano mbalimbali ikiwemo ya kimataifa. Endapo atajiunga na timu hiyo, atakuwa mchezaji wa pili wa Yanga kucheza Afrika ya Kusini, baada ya Mrisho Ngasa kuripotiwa kujiunga na Free State mwezi July mwaka huu
Post a Comment