Rais Pierre Nkurunziza
Rais wa
Burundi, Pierre Nkurunziza, inasemekana ameondoka nchini Tanzania saa
moja baada ya kupatikana taarifa za kupinduliwa kwake na kiongozi mkuu
wa majeshi yake Meja jenerali Godefroid Niyombare kutangaza kwamba
amempindua.
Jenerali
huyo mara baada ya tangazo lake, akaweka amri ya kufungwa kwa kiwanja
cha kimataifa cha ndege nchini humo ikiwemo mipaka ya Burundi.
Hata hivyo
haiko wazi ikiwa jeshi linamuunga mkono Meja jenerali Godefroid
Niyombare. Naye msemaji wa rais wa Burundi, amesema kwamba wanajeshi
watiifu kwa Rais ambaye alikuwa akihudhuria mkutano wa viongozi nchini
Tanzania, amesema nchi iko shwari.
Maelfu ya
watu wamekuwa katika shamra shamra katika mji mkuu wan chi hiyo
Bujumbura baada ya wiki kadhaa za maandamano kumpinga katika maamuzi
yake ya kugombea muhula wa tatu wa uongozi,na tayari mpaka sasa viongozi
wakuu wa kanda wamelaani mapinduzi hayo.
Mgogoro wa Burundi umezusha wasi wasi wa kurejea katika ghasia baada ya miaka kumi na miwili ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Zaidi ya
watu elfu tatu walikufa katika vita vya kikabila kati ya wahutu na
watutsi ,vita vilivyomalizwa muongo uliopita.na mgogoro wa sasa nchini
humo umehusisha kwa kiasi kikubwa na masuala ya kisiasa.
lakini,yaliyojiri Burundi hayana tofauti na kilichojiri katika nchi
jirani ya Rwanda ambayo ilikumbwa na mauaji ya kimbari nayo ilikabiliwa
na masuala ya ukabila.
Umoja wa
mataifa umeonya hivi karibuni kwamba ikiwa ghasia zitasitishwa Burundi
itakuwa na Amani na kama itakuwa vinginevyo basi nchi hiyo itarejea
katika vita vya wenyewe kwa wenyewe .
CREDIT: BBC
Post a Comment