0


fifa_web-jpg20150527101508
  • Mwanasheria mkuu wa Marekani amesema watuhumiwa walitaka wafaidike na soko la soka la Marekani linalokua.
  • Chuck Blazer (moja wa mabosi wa soka la Marekani) alikuwa mtoa taarifa wa waendesha mashitaki wa Marekani
  • Michael Garcia, aliyewahi kuwa mwanasheria wa Marekani mara moja, alipewa kazi ya kuangalia mchakato mzima wa kuzawadia nchi kuandaa mashindano.
Katika miaka ya karibuni, FIFA imekuwa ikitengeneza habari sio tu kwa kuhakikisha sheria za mpira zinasimamiwa bali pia chombo hiki kikubwa kinachoongoza mpira wa miguu duniani, kuzivunja sheria pia.
Taasisi hii inayoongoza kabumbu, mchezo maarufu zaidi duniani, ni kama mnyama mbaya mwenye thamani ya mabilioni ya dola.
FIFA imekuwa ikishutumiwa vikali mara kwa mara kujihusisha na rushwa. Shutuma ambazo zilizidi zaidi pale walipoizawadia Russia na Qatar kuandaa kombe la dunia mwaka 2018 na 2022.
Baada ya hilo kusemwa sana, FIFA ilijifanyia uchunguzi yenyewe na kujisafisha.
Lakini ni kwa nini Marekani, taifa ambalo soka halipewi kipaumbele sana kama mpira wa kikapu, sasa linawapeleka viongozi wa juu wa FIFA mahakamani kwa sababu ya ufisadi?
Kati ya watu kumi na nne waliotajwa, wengi si Wamarekani.
Lakini kama Mwanasheria Mkuu wa Marekani, Loretta Lynch anavyoliweka bayana suala hili anasema, watuhumiwa walipanga uhalifu wao wakiwa Marekani; walitumia mfumo wa kibenki wa Marekani, walipanga kutajirika kupitia mpango uliolenga soko la soka linalokua Marekani.
Ili uelewe hili, tutakuonesha ni jinsi gani Wamarekani wanahusika katika kila steji.
 
Mwanzo …
Michael Garcia:
Kombe la Dunia ni kitu kikubwa. Linakuja kila baada ya miaka minne. Na kila linapokuja inakuwa ni shindano la michezo linalofuatiliwa zaidi kwenye sayari.
FIFA ilipowazawadia Russia kuandaa michezo ya mwaka 2018 na kufuatiwa na hatua nyingine inayochanganya kichwa zaidi kwa kuwapa Qatar kuandaa mwaka 2022, wakosoaji na serikali zingine walilalamika kuchezewa faulo. Walitaka mchakato mzima wa kuzawadia Qatar na Russia uwekwe wazi.
Soma ripoti
FIFA walimleta Michael Garcia, huyu aliwahi kuwa mwanasheria wa Marekani mara moja wilaya ya kusini (Southern Distritct) ya New York. Alipewa kazi ya kuangalia tabia ya nchi hizo mbili.
Alitumia miezi 19 kuchunguza jinsi mchakato mzima ulivyofanyika.
Mpaka anamaliza, mambo yote aliyogundua yalikuwa kwenye kurasa 350.
Ni nini FIFA walifanya?
Waliificha ripoti ile, nakutoa taarifa yao yenye kurasa 42 – na kujisafisha kwamba hakuna kosa lolote lililofanyika. Hiyo ilikuwa mwezi Novemba.
Garcia hakukubali. Alisema ile taarifa  iliyotolewa na FIFA, haijakamilika na ina makosa kibao.
 
Baada ya hapo, tunakuletea;
James Comey na Loretta Lynch:
Kama tulivyosema mwanzo, Garcia alikuwa Mwanasheria wa Marekani, katika wilaya ya kusini ya New York. Mtu aliyekuwa akiishika ofisi hiyo kabla yake anaitwa James Comey.
Kwa sasa ni Mkurugenzi wa FBI. Na hizi shutuma za uhalifu wa rushwa ni matokeo ya miaka mitatu ya uchunguzi wa FBI.
Pia kuna mtu mwingine kutoka New York. Huyu ni Mwanasheria Mkuu wa Marekani, Loretta Lynch.
Aliiona kesi hii kipindi akiwa yupo Brooklyn kabla hajachaguliwa kuongoza Kitengo hicho cha Sheria.
Lakini kwa nini watu wa Marekani waanze kuifuatilia FIFA?
Wakati FIFA inajisafisha, FBI haikuwa tayari kufanya hivyo.
Walitaka kujua kama shutuma za kupokea rushwa za watu wa FIFA zilifanyika katika ardhi ya Amerika.
 
Chuck Blazer
Chuck Blazer, Mmarekani, alikuwa ni mtu wa pili kwa cheo, CONCACAF, taasisi inayoshirikiana na FIFA kuendesha na kusimamia mpira Amerika ya kaskazini na Karibiani. Makao yake makuu yapo Florida.
Blazer amejikuta matatani kutokana na kuwa na Dola 11 Milioni, ambazo hazijulikani chanzo chake, kulingana na ripoti ya IRS (chombo kinachosimamia mapato nchini Marekani). IRS ilisema Blazer hajalipa kodi kwa miaka mingi sana.
Alikutwa na hatia ya makosa ya ufisadi mwaka 2013, hivyo alikuwa akivalishwa waya maalum na FBI kwa ajili ya uchunguzi wao. Alitoa nyaraka mbalimbali na rekodi za FIFA kwa FBI.
Unakumbuka tulipoitaja CONCACAF? Marekani pia ipo ndani yake.
Huku wakiwa na Blazer kama mshirika na shahidi wao katika hili. FBI walitaka kujua kama kulikuwa na ufisadi wowote ndani ya mashindano yaliyoandaliwa ndani ya Amerika. FBI wanasema ni kweli ufisadi ulikwepo.
Moja ya watu wengine ambao wapo matatani hivi sasa ni Jeffrey Webb. Huyu ni makamu wa Rais wa FIFA na ndiye aliyekuwa anaiongoza CONCACAF (Mpaka jana alipositishwa) na pia alikuwa ni bosi wa Blazer.
Webb alitumia nafasi yake kufanya vitendo vya rushwa na mabosi wa masuala ya masoko. Kwa malipo ya kupata matangazo ya televisheni, masoko na udhamini wa mechi zote ndani ya Amerika.
Waendesha mashitaka wanasema, wale waliokamatwa walikubali kupokea rushwa yenye thamani ya zaidi ya Dola 100 Milioni kuanzia mwanzoni mwa miaka ya 1990 mpaka sasa.
Kwa mfano, Dola 110 milioni za rushwa zitumike kuhamisha Copa America, mashindano ya soka, ambayo kawaida huandaliwa Amerika ya Kusini, kupelekwa Marekani mwaka 2016, alisema Lynch.
Lakini je ni kweli Marekani inaweza kuwakamata viongozi wa FIFA? Jibu ni, Ndiyo kwa sababu ndicho wanachofanya hivi sasa.
 
Marekani:
Marekani iliamua kuwafungulia kesi watuhumiwa kwa sababu mambo yote hayo yalifanyika ndani ya ardhi yao.
“Kulingana na ombi la Marekani, uhalifu huu ulikubaliwa na kuandaliwa ndani ya Marekani, na malipo yalifanyika kwa kutumia benki za Marekani.” Ilisema ofisi ya sheria nchini Uswisi.
Waendesha mashitaka walisema pia kwamba  kanuni za  kodi na benki za Marekani zilisaidia katika kufungua mashitaka hayo.
Kwa kuongeza, mamlaka za Marekani zina mamlaka ya kisheria katika hili kwa sababu soko la televisheni la Marekani na mabilioni ya dola yaliyolipwa na mitandao yao ni kubwa sana katika Kombe la Dunia.

Post a Comment

 
Top