Wakazi wa Mkuyuni jijini Mwanza wakiwa katika eneo alilotupwa mtoto wakisubiri polisi.
Polisi akishirikiana na wananchi kuuchukua mwili wa mtoto huyo katika jalala alipotupwa na mama yake mzazi.
...wakisaidiana kuubeba mwili wa mtoto.
...wakielekea kwenye gari la jeshi la polisi.
...wakiupakiza mwili kwenye gari la jeshi la polisi.
...wananchi wakitaharuki kutokana na kitendo hicho cha mama kumtupa mwanaye dampo.
Mwili wa mtoto huyo ukiwa kwenye gari la polisi.
...gari la polisi likiondoka katika eneo la tukio.
...wananchi wakisambaa kutoka kwenye eneo la tukio.
Wananchi wakijadiliana baada ya tukio hilo.
Na Johnson James, GPL / Mwanza
MAMA
mmoja mkazi wa kata ya Mkuyuni-Sokoni wilayani Nyamagana jijini Mwanza
(jina lake halikufahamika mara moja) amejifungua mtoto wa kiume na kisha
kumtupa kwenye shimo la kutupa taka (jalala) eneo a Mkuyuni jijini
hapa.
Akizungumza
na waandishi wa habari, mmoja wa watoa taarifa kwa viongozi wa serikali
aliyetoa sharti la kutotajwa jina lake amesema:
“Mimi ni
mfanya usafi hapa Mkuyuni, wakati ninaenda kumwaga uchafu pale dampo
nikakuta kitoto kichanga kimetupwa maeneo hayo ndipo nilipoenda kutoa
taarifa kwa Mwenyekiti wa Mtaa wa Mkuyuni-Sokoni ili wafanye utaratibu
wa kukitoa hapo:”
Naye
mwenyekiti wa mtaa wa Mkuyuni, Godwin Peter Kyangara, amesema: “Mimi
nimeletewa hizi taarifa za mtoto huyu aliyetupwa maeneo haya mida ya saa
2:30 asubuhi, baada ya kupokea taarifa hizo ikabidi nikatoe taarifa kwa
Jeshi la Polisi ndipo walipokuja kuuchukua mwili wa mtoto huyo.”
Inasemekana
kwamba mtoto huyo alikuwa tayari ana umri wa miezi tisa hivyo mzazi
wake alikuwa tayari amejifungua ndipo alipoamua kumtelekeza kwenye shimo
hilo la kutupa takataka.
Kwa
upande wake, diwani wa kata ya Mkuyuni, Charles Fashion, ameeleza kuwa
ameshangazwa na kitendo hicho cha mwanamke kujifungua mtoto na kumtupa
jalalani ambapo alisema inabidi atafutwe na apewe adhabu iwe fundisho
kwa akina mama wengine wenye tabia kama hizo katika jamii.
Post a Comment