SIKU YA HAFLA MAALUM KWA WALEMAVU ILIYOFANYIKA WILAYANI LIWALE MKOANI LINDI SIKU YA TAREHE 29/3/2015 (PICHA KWA HISANI YA MDAU WETU)
Na mwandishi wetu Liwale-Lindi
Kitengo cha
ustawi wa jamii,wilaya Liwale mkoa wa Lindi kimakabiliwa na changamoto
mbalimbali ikwemo kutokuwa na bajeti ya fedha hali inayofanya washindwe kufika
vijijini ili kutathimini matukio ua vitendo vya ukatili na unyanyasaji wa
kijinsia.
Hayo yamebainisha kwenye hafla maalum kwa ndugu zetu wenye ulemavu iliyofanyika wiki iliyopita tarehe 29/3/2015 na ofisa ustawi wa jamii wilaya Liwale Freddy Magelasa kwenye Tafrija
ya watu wenye ulemavu iliyoandaliwa na mkuu wa wilaya hiyo .
Magelesa alisema changamoto kubwa inayoikabili kitengo cha ustawi wa jamii
wilayani humo katika kutekeleza majukumu
yake ni ukosefu wa fedha kwa ajili yakusimamia na kutekeleza wa kazi hizo.
Jamii inatulaumu kwa
kutofika kwenye matukio ,ukweli mazingira si rafiki, kutokana na kukosa fedha za uendeshaji alisema
Magelesa.
Kwa upande wake katibu
wa chama walemavu wilaya Liwale Saidi Jika alisema matukio
ya,kunyanyasika,walemavu akina mama na watoto,kubakwa na kutelekezwa kimajukumu
yamekuwa yakijitokeza kila wakati kutokana na jamii kutoelewa athari za matuki
hayo kwa sasa na siku za usoni na kuiomba serikali kuyatafutia ufumbuzi
Post a Comment