0

  1. Mwenyekiti wa Tume ya Uchunguzi kuhusu operesheni tokomeza Jaji(Mstaafu) Balozi Hamisi Amiri Msumi akimkabithi Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete Ripoti ya Uchunguzi wa Tume hiyo katika hafla fupi iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam leo.Rais Kikwete aliiteua tume hiyo mwaka jana kuchunguza tuhuma za uvunjifu wa sheria katika utekelezaji wa operesheni hiyo








  2. PRESIDENT’S OFFICE,
  3. STATE HOUSE,
  4. 1 BARACK OBAMA ROAD, 
  5. 11400 DAR ES SALAAM.
  6. Tanzania.





  7. TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
  8. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Ijumaa, Aprili 10, 2015 amepokea Ripoti ya Uchunguzi wa Operesheni Tokomeza katika halfa fupi ilifanyika Ikulu, Dar es Salaam.
  9. Mara baada ya kupokea Ripoti hiyo, Rais Kikwete ameishukuru Tume kwa kazi nzuri na kuongeza kuwa amefurahi kuwa suala zima la Operesheni Tokomeza sasa limefika mwisho wake.
  10. Aidha, Rais amesema kuwa Serikali itaisoma Ripoti hiyo na katika wiki mbili itatoa maelezo ya jinsi Ripoti hiyo itakavyoshughulikiwa.
  11. Rais Kikwete amepokea Ripoti hiyo kutoka kwa Balozi Jaji (mstaafu) Hamisi Amiri Msumi, Mwenyekiti wa Tume ambayo Rais Kikwete aliiteua Mei Mosi, mwaka jana, 2014, na kuitaka ichunguze tuhuma mbali mbali za uvunjifu wa Sheria, Kanuni, Taratibu na Hadidu za Rejea za Utekelezaji wa Operesheni Tokomeza.
  12. Aidha, Rais Kikwete aliipa Tume hiyo jukumu la kupendekeza hatua stahiki za kisheria za kuchukua dhidi ya watakaobainika kuhusika na uvunjifu huo. Vile vile, Rais aliiagiza Tume hiyo ishauri namna bora ya utekelezaji wa Operesheni kama hiyo hapo baadaye.
  13. Rais Kikwete pia aliipa Tume hiyo Hadidu za Rejea sita ambazo pia ziliainishwa katika Taarifa ya Serikali Nambari 131 ya 2014. Hadidu za Rejea hizo ni kama zifuatazo:


  14. (a) Kuchunguza namna Operesheni Tokomeza ilivyotekelezwa;
  15. (b) Kuchunguza iwapo maafisa waliotekeleza Operesheni Tomokeza walizingatia sheria, kanuni, taratibu na hadidu za rejea walizopewa;
  16. (c) Kuchunguza iwapo maofisa waliotekeleza Operesheni Tokomeza walivunja sheria, kanuni, taratibu na hadidu rejea walizopewa.
  17. (d) Kuchunguza iwapo kuna watu waliokiuka sheria yoyote wakati wa utekelezaji wa Operesheni Tokomeza na iwapo hatua zilizochukuliwa na maofisa wa Operesheni Tokomeza dhidi ya wakosaji hao na mali zao zilikuwa sahihi;
  18. (e) Kupendekeza hatua zinazostahili kuchukuliwa dhidi ya maafisa wa Operesheni Tokomeza waliokiuka sheria, kanuni, taratibu na hadidu za rejea za Operesheno Tokomeza; na
  19. (f) Kupendekeza mambo yanayopaswa kuzingatiwa wakati wa kupanga na kutekeleza Operesheni nyingine kama hii, ili kuepuka malalamiko mengine yasitokee.
  20. Jaji Msumi amemweleza Rais Kikwete kuwa katika kutelekeza majukumu yake, Tume ilitembelea mikoa 20 na wilaya 38 na kupokea malalamiko mbali mbali kutoka kwa wafuatao:
  21. (a) Viongozi wa Serikali ikiwa ni pamoja na mawaziri wanne waliojiuzulu kutokana na sakata hilo;
  22. (b) Watekelezaji wa Operesheni; na
  23. (c) Walalamikaji/wahanga wa Operesheni.
  24. Jaji Msumi amemweleza Rais Kikwete kuwa Ripoti ya Tume ina Juzuu kumi, Juzuu ya kwanza ikiwa ni Muhtasari wa Taarifa ya Tume, Juzuu ya pili ikiwa ni Taarifa yenyewe ya Tume, Juzuu ya tatu hadi ya tisa ikiwa ni Mwenendo wa Ushahidi (Proceedings) na Juzuu ya kumi ikiwa ni vielelezo vilivyotolewa na mashahidi.
  25. Mwisho.
  26. Imetolewa na;
  27. Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
  28. Ikulu – Dar es Salaam.
  29. 10 Aprili, 2015


  30. Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Tume ya Uchunguziwa operesheni Tokomomeza ikulu leo.(picha na Freddy Maro.

Post a Comment

 
Top