Kaunti
ya Elgeyo Marakwet nchini Kenya inakabiliwa na changamoto kubwa ya
wauguzi katika kituo cha Afya cha Simbeiwe, lakini changamoto hiyo
inatokana na ishu ambayo imelalamikiwa sana na wahudumu wa afya ambao
huwa wanapelekwa maeneo hayo.
Wahudumu wanaopangiwa kufanya kazi
katika kituo hicho wanalalamika kwamba eneo hilo lina matukio ambayo
yanahusishwa na imani za kishirikina.
Mmoja wa wauguzi aliyeacha kazi katika
kituo hicho anasema alikutana na maajabu ya zimwi lililomning’iniza
mtoto mdogo hewani bila kumshika wakati alipokuwa akijitayarisha
kumchoma sindano mtoto huyo.
Waziri wa Afya katika kaunti hiyo, Thomas Ruto amesema wanatafuta wahudumu wa afya ambao wataweza kuhimili kazi katika mazingira kama hayo.
Kiongozi mwingine amepingana na taarifa
kwamba kuna ishu ya uchawi kuwepo maeneo hayo, anasema uchawi
ulikuwepo zamani ila kwa sasa haupo.
Post a Comment