Watu
42 wamepoteza maisha na wengine kujeruhiwa vibaya baada ya basi
walilokuwa wakisafiria mali ya kampuni ya Majinja lenye bnamba za
usajili T438 CED kuangukiwa na kontena baada ya kugongana na lori la mizigo Scania
namba T 689 APJ, mali ya Cipex Company katika eneo la Changarawe, nje kidogo ya mji wa Mafinga mkoani Iringa Jana.
Basi hilo lilikuwa likitokea mkoani Mbeya kwenda Dar es Salaam huku lori likitoka Dar es Salaam kwenda Mbeya.
Basi hilo lilikuwa likitokea mkoani Mbeya kwenda Dar es Salaam huku lori likitoka Dar es Salaam kwenda Mbeya.
Ubovu
wa barabara katika eneo hilo inaelezwa kuwa chanzo cha ajali hiyo
ambacho kilichangiwa na mwendo kasi wa madereva na kutopeana mnafasi ya
kupita eneo lenye mashimo.
Vyombo
vya uokoaji yakiwemo magreda yalifika katika eneo la tukio na kulitoa
kontena hilo na shughuli za uopoaji wa maiti kufanyika kwa wananchi
wakishirikiana na wanajeshi wa JKT Mafinga na askari wengine.
Basi hilo linadaiwa kuanza safari jijini Mbeya likiwa na abiria 37 lakini hadi wanafika eneo la ajali lilikuwa na abiria 64.
Post a Comment