Licha ya wadau wa habari kuwasilisha ombi kwa Spika wa Bunge, Anne Makinda wakitaka miswada miwili ya habari ya mwaka 2015 iwasilishwe kwa mfumo wa kawaida, Serikali imeing’ang’ania huku ikisema itawasilishwa chini ya hati ya dharura Jumanne ijayo.
Miswada hiyo ni kati ya minne yenye ‘utata’ ambayo
ilikuwa iwasilishwe bungeni leo na kesho, lakini jana ofisi ya Bunge
ilitoa ratiba mpya inayoonyesha kuwa itawasilishwa wiki ijayo chini ya
hati ya dharura, ikiwa ni kinyume na maombi ya wadau wa habari.
Kaimu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Tundu
Lissu aliliambia gazeti hili jana kwamba Serikali inataka kufanya ubabe
na imepanga kuiwasilisha Jumanne asubuhi licha ya wabunge kutojua nini
kimeandikwa.
Miswada hiyo ni pamoja na ule wa Sheria ya Miamala
ya Kielektroniki wa mwaka 2014, Muswada wa Sheria ya Makosa ya Mtandao
wa mwaka 2015, Muswada wa Sheria ya Kupata Habari wa mwaka 2015 na
Muswada wa Sheria ya Vyombo vya Habari.
Juzi, wadau hao walimwomba Spika Makinda atumie
hekima kuishauri Serikali iiwasilishe katika mfumo wa kawaida miswada
miwili ya habari, ili kutoa fursa kwa wananchi na wadau kutoa maoni
kabla ya kupitishwa na kuwa sheria.
Imeelezwa kuwa Jumanne, Muswada utakaoanza
kuwasilishwa bungeni ni ule wa Sheria ya Kupata Habari na utafuatiwa na
wa Sheria ya Vyombo vya Habari.
“Tunajua kuwa miswada hii imelenga kuvifungia
vyombo vya habari, maana huu ni mwaka wa uchaguzi. Wanachokifanya
Serikali ni kuiwasilisha bungeni ‘kimafia’ tu. Sisi tutakachokifanya ni
kuibana bungeni,” alisema Lissu.
Hata hivyo, alisema kutokana na wingi wa wabunge
wa CCM, huenda miswada hiyo ikapitishwa, jambo alilodai kuwa litakuwa
gumu kulizuia.
“Mpaka sasa hatujaipata miswada hii, kwa kweli jambo hili linatusikitisha maana hata katika kamati haijafika,” alisema Lissu.
Tangu mkutano wa 19 wa Bunge unaoendelea mjini
hapa ulipoanza, kumekuwa na taarifa kuwa Serikali inakusudia kuwasilisha miswada hiyo chini ya hati ya dharura,
lakini wadau wa habari wameendelea kuiomba ibadili msimamo huo kwani
kufanya hivyo kutawanyima wananchi fursa ya kutoa maoni juu ya miswada
hiyo kabla ya kuwa sheria.
Kaimu Katibu wa Bunge, John Joel juzi alilieleza
gazeti hili kuwa miswada hiyo hata ikiwasilishwa itakuwa vigumu
kujadiliwa kutokana na muda uliopo, huku akishindwa kuthibitisha kama
kweli itawasilishwa ama laa.
Alipotafutwa tena jana, Kaimua Katibu huyo wa
Bunge, Joel kufafanua mabadiliko ya ratiba hiyo na kama miswada hiyo
pamoja na hati ya dharura vimeshafikishwa katika ofisi ya Spika,
hakupatikana.KUENDELEA BOFYA HAPA
inakusudia kuwasilisha
miswada hiyo chini ya hati ya dharura, lakini wadau wa habari
wameendelea kuiomba ibadili msimamo huo kwani kufanya hivyo kutawanyima
wananchi fursa ya kutoa maoni juu ya miswada hiyo kabla ya kuwa sheria.
Kaimu Katibu wa Bunge, John Joel juzi alilieleza
gazeti hili kuwa miswada hiyo hata ikiwasilishwa itakuwa vigumu
kujadiliwa kutokana na muda uliopo, huku akishindwa kuthibitisha kama
kweli itawasilishwa ama laa.
Alipotafutwa tena jana, Kaimua Katibu huyo wa
Bunge, Joel kufafanua mabadiliko ya ratiba hiyo na kama miswada hiyo
pamoja na hati ya dharura vimeshafikishwa katika ofisi ya Spika,
hakupatikana.
Post a Comment