Wakizungumza na waandishi wa habari wanajeshi hao zaidi ya elfu moja walioko katika mkoa wa Dar es Salaam wamelalamika uamuzi wa serikali wa kutumia makampuni binafsi kulinda taasisi zake na kuwahacha wakiwa hawana ajira wakati wamefanya mafunzo ya kijeshi kwa gharama kubwa za serikali kwa miaka miwili ikiwemo matumizi ya silaha na kutelekezwa mitaani.
Akizungumza na waandishi wa habari makamu mwenyekiti wa umoja wa wanajeshi wa JKT walioko mitaani, Parali Kiwango amesema gharama za kuwahacha askari uraini katika maisha magumu na mazingira yasiyo rafiki ni kubwa kuliko raia kwa kuwa wanaweza kushawishika na kufanya maamuzi magumu.Source:ITV
Post a Comment