Kama ulikuwa unashangaa refa wa Toto dhidi ya
Polisi Tabora akikimbizwa kama mwizi, sasa zamu ya kushangaa michuano ya Kombe
la Mataifa Afrika.
Mwamuzi wa mchezo kati ya wenyeji Equatorial
Guinea dhidi ya vigogo Tunisia aliishia kukimbizwa na wachezaji wa Tunisia
wakitaka kumdunda.
Wachezaji hao walisai mwamuzi huyo alitoa penalti
kwa wenyeji na haikuwa penalti na wenyeji hao wakafunga na kusababisha mechi
iongezwe dakika 30 na mwisho wakaishia kushinda 2-1 na kuwatoa Tunisia.
Mara baada ya mechi, mwamuzi huyo alikuwa katika
wakati mgumu huku wachezaji wa Tunisia wenye jazba kama nyati wakimkimbiza.
Polisi na walinzi wa uwanjani hapo walilazimika
kufanya kazi ya ziada kumuokoa. Ehh!

Post a Comment