Hatimaye
timu nane zitakazocheza robo fainali za Kombe la FA huko England
zimejulikana baada ya kukamilika kwa michezo ya kufuzu kucheza hatua
hiyo.
Mabingwa watetezi wa kombe la FA, Arsenal itapambana na
Manchester United katika hatua hiyo ya nane bora. Arsenal watasafiri
kwenda Old Trafford kuikabili Manachester United katika mchezo wa robo
fainali zitakazochezwa tarehe 7 au 8 ya mwezi Machi.Manchester United ilijihakikishia nafasi hiyo ya hatua ya nane bora baada ya kuishindilia Preston North End mabao 3-1.
Liverpool itakuwa mwenyeji wa Blackburn, Bradford City itapambana na Reading wakati wapinzani wa jadi kutoka West Midlands Aston Villa na West Brom zitamenyana katika uwanja wa Villa Park.
Hatua ya robo fainali kwa timu ya Liverpool itampa matumaini nahodha wake Steven Gerrard kucheza fainali katika uwanja wa Wembley ukiwa ni msimu wake wa mwisho kuwa katika kikosi cha Liverpool, japokuwa watatakiwa kuishinda Blackburn ambao tayari waliwatoa nje ya kinyang'anyiro cha kombe la FA Swansea na Stoke timu za ligi kuu ya England msimu huu.
Ratiba ya michezo ya robo fainali za kombe la FA inaonyesha kuwa:
Aston Villa watapambana na West Brom, Bradford City na Reading, Liverpool watakuwa kibaruani na Blackburn, huku Manchester United wakipimana ubavu na mabingwa watetezi wa kombe hilo, Arsenal. Michezo hiyo itachezwa katika siku za mwisho wa juma tarehe 7 na 8.
Post a Comment