
MBOWE KAISHINDA CCM.
Akiwa mwenye kiti wa CHADEMA yeye ndiye kiongozi wa ngazi ya juu kabisa ya chama. Hivyo kwabusara zake na kutoa fursa sawa kwa wote amefanya yafuatayo.
Kafuta dhana ya chama Mbowe?
Mbowe amefuta ile dhana iliyopandikizwa na maccm kuwa CHADEMA ni chama cha Mbowe na wakatumia sana kuwakatisha tamaa watanzania waliokuwa na myoyo midogo kwa wakati ule. ccm walijaribu kuunga unga hadithi na kuonesha uhusiano wenye afya uliopo kati ya Mbowe na Mwasisi wa CHADEMA MZEE MTEI
KAFUTA DHANA YA CHADEMA KUWA CHAMA CHA KASKAZINI.
Pamoja na wabunge wengi wa chadema kutoka kanda ya ziwa lakini bado ccm walikazania kusema chadema ni chama cha kaskazini.Mbowe kama mwenyekiti ametimiza wajibu wake leo CHADEMA NI YA KITANZANIA NA CCM WANAJUA HILO.
KAFUTA DHANA YA CHADEMA KUWA CHAMA CHA KIDINI.
Mbowe kama mwenyekiti wa chama amepita katika kipindi kigumu cha kupambana na maccm juu ya udini. Kutokana na yeye na wanachama kukubali Dr slaa agombee urais kupitia chadema na kwakua historia ya Slaa imebebwa pia na utumishi uliotukuka katika kanisa basi maccm walimua kusema Chadema ni chama cha kikristo. Hili nalo limepita.
KAFUTA DHANA YA CHAMA KUWA CHA KIGAIDI.
Mbowe kama mwenyekiti wa chama alisimama kidete kupambana ma hila za ccm na mawakala wake kusema CHADEMA ni chama cha kigaidi. Pamoja na nguvu ya kifedha waliotumia akina Mwigulu bado hila hizo hazikufua dafu. kilikua kipindi kigumu sana kwa mwenyekiti lakini aliendelea kukomaa.
YAPO MENGI SANA LAKINI KAMA DHANA YA UKABILA NA MENGINE AMBAYO AMEPAMBANA NAYO NA SASA CHAMA KIKO IMARA.
KWA WALE WANAOPATA BAHATI YA KUHUDHURIA VIKAO ANAVYO KUWEPO MBOWE, AU WANAO FUATILIA AKIWA ANACHANGIA BUNGENI UTAKUA UMEAMINI KUWA MBOWE WA LEO SI YULE WA MWAKA 1995.
NA LAZIMA TUAMINI KUWA KILA INAPO ITWA LEO MBOWE ANAZIDI KUWA MTU MAKINI NA KIONGOZI IMARA SANA.
MBOWE NI MWENYEKITI WA PILI KWA UIMARA KUTOKA KWA NYERERE .
SASA ANAIFUTA CCM.
Lazima tuamini kuwa kwasasa baada ya kupambana na hayo yote kibao kimegeuka na sasa ccm ndiyo wanapata tabu maana hali yao imekua ngumu sana MBOWE NA SAFU NZIMA YA UONGOZI NDANI YA CHADEMA IMEDHAMIRIA KUOINDOA CCM TANZANIA.
Niishie hapo kwa kuwashukuru nyote mnao unga mkono CHADEMA maana ninyi ni wapenda mabadiliko chanya ya Taifa hili.
Wako;
Philipo Mwakibinga
M/kit CDM BAVICHA CHUNYA
M/KIT CDM TAWI UDOM.
Post a Comment