Upepo mkali umeezua paa za nyumba 27 katika kijiji cha Namtumbwa na Mbaya,Kata ya Mbaya katika Tarafa ya Liwale Wilayani Liwale na kusababisha hasara kubwa kwa wananchi.
Wakizungumzia tukio hilo, wananchi walisema upepo huo ulivuma kwa kasi kubwa siku ya jumatatu kumkia jana jumanne.Baadhi ya nyumba zilizoezuliwa ni Zahanati,nyumba ya walimu wa shule ya msingi,ofisi ya ccm,familia ya Mchungulike nyumba 3,familia ya Mpitage nyumba 3,nyumba zingine kwa mzee bin Ali kipeleka,Abdala Ngalemba,Mandela,Hashimu Mkarapi,mzee Mnange,mzee Mnagilage,Rashidi Kiwanga,Mohamedi Kamaliza,Mzee Zawadi,Kilengeo,Mangi,Mzee Shaibu Muharo,Libaja,Mengunike,Jafari Mtende,Ligou na Mnyaru.
Hizo ni baadhi ya nyumba zilizoezuliwa paa za nyumba siku ya jumatatu kuamkia jana katika vijiji viwili ambapo vijiji hivyo zamani kulikuwa ni kijiji kimoja kilichojulikana Mbaya.
Post a Comment