Dar es Salaam. Kamati iliyoundwa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), kuchunguza mabilioni ya fedha yaliyofichwa na baadhi ya Watanzania katika benki mbalimbali nchini Uswisi, imekamilisha uchunguzi na inasubiri kukabidhi ripoti ya kazi hiyo kwa Spika wa Bunge.
Hayo yalisemwa jana na Mwanasheria Mkuu wa
Serikali, George Masaju alipokuwa akizungumza na wahariri wa vyombo
mbalimbali vya habari, Dar es Salaam.
Masaju alisema kamati hiyo ilikamilisha kazi yake
baada ya kuwahoji watu mbalimbali na kukamilisha kazi hiyo kama
walivyoagizwa na Bunge na kinachosubiriwa ni kuikabidhi kwa chombo hicho
cha kutunga sheria.
“Ofisi yangu kupitia kamati iliyoundwa
tulikwishamaliza kazi hii, lakini hatuwezi kutoa taarifa kupitia sehemu
nyingine zaidi ya ofisi iliyotupatia kazi kama utaratibu unavyoelekeza.
“Sasa wananchi na nyie waandishi wa habari msubiri
taarifa hiyo itolewe kule bungeni ambako tuhuma hizi zilianzia,”
alisema Masaju.
Watuhumiwa
Vigogo 10 wametajwa kuhusika katika kashfa hiyo.
Inadaiwa kuwa katika orodha hiyo, yupo kiongozi mmoja mwandamizi
mstaafu, maofisa watatu wastaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania
(JWTZ), mawaziri wastaafu ambao baadhi yao bado ni wabunge na aliyewahi
kuwa kiongozi mwandamizi wa Benki Kuu Tanzania (BoT).
Kamati ilivyoundwa
Kamati hiyo maalumu iliundwa kwa Azimio la Bunge
baada ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe kuibua tena tuhuma hizo
bungeni mapema mwaka jana, akidai kuna vigogo walioficha Sh323.4
bilioni katika benki mbalimbali za Uswisi.
Kiasi hicho cha fedha kinaweza kujenga barabara ya
lami yenye urefu wa kilomita 300 ambao ni sawa na kutoka Morogoro hadi
Iringa.
Kwa mara ya kwanza, tuhuma hizo zilitolewa bungeni
na Zitto ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za
Serikali (PAC), mwaka 2012.
Katika kikao cha Tisa cha Bunge, Zitto
aliwasilisha hoja binafsi kulitaka Bunge kuchunguza na kuielekeza
Serikali kuchukua hatua dhidi ya Watanzania aliowaita vigogo walioficha
fedha na mali haramu nje ya nchi.
Kutokana na hoja hiyo, Bunge chini ya Spika Anne Makinda,
liliipa Serikali muda wa mwaka mmoja ambao ulimalizika Oktoba mwaka jana
iwe imekamilisha uchunguzi na kuwasilisha ripoti yake bungeni.
Wakati sakata hilo lilipokuwa limepamba moto,
Serikali ya Uswisi kupitia kwa Balozi wake nchini, Olivier Chave iliwahi
kusema Serikali ya Tanzania haijaonyesha nia ya dhati kutaka kuchunguza
na kurejesha mabilioni ya fedha hizo.
Balozi Chave alikaririwa wakati huo akisema
hawajaona jitihada zozote zilizofanywa na Serikali ya Tanzania kutaka
kuzipatia ufumbuzi tuhuma hizo.
Chave alisema nchi yake iko tayari kushirikiana na
Tanzania kujua uhalali wa fedha hizo na endapo zitagundulika ni chafu
watakuwa tayari kuzirejesha nchini.
Taarifa kutoka Benki Kuu ya Uswisi inaonyesha kuwa
baadhi ya fedha hizo zimewekwa katika akaunti za vigogo hao na kampuni
za mafuta na gesi zilizopo nchini.
Hata hivyo, Machi mwaka jana ilielezwa kuwa
mabilioni ya shilingi yaliyowekwa na Watanzania katika benki za Uswisi
yalikuwa yameanza kuhamishwa kimyakimya.
Ripoti ya Benki za Uswisi ya 2012 ilionyesha kuwa
fedha zinazotoka Tanzania zilipungua kwa karibu Sh36.4 bilioni
ikilinganishwa na zilizokuwapo 2011 nchini humo, lakini haielezi sababu
ya kupungua kwake.
Watanzania 99
Hivi karibuni, Timu ya Wanahabari wa Kimataifa
wanaoandika Habari za Uchunguzi (ICIJ) ilitoa ripoti ikisema Watanzania
99 wanamiliki Dola za Marekani 114 milioni (Sh193bilioni) kwenye akaunti
za benki nchini Uswisi.
Ripoti hiyo inayoitwa SwissLeaks iliyotolewa
Marekani, imesheheni taarifa za Benki ya HSBC ya Uswisi na namna watu
maarufu wakiwamo wanasiasa, wachezaji, viongozi wa dini na
wafanyabiashara walivyoficha mamilioni ya fedha na kufanikiwa kuzikwepa
mamlaka za mapato katika nchi zao.
Katika orodha hiyo, Tanzania inashika nafasi ya
100 duniani na nafasi ya pili Afrika Mashariki ikiwa nyuma ya Kenya
inayoshika nafasi ya 58 duniani kwa kuweka zaidi ya Sh950 bilioni nchini
Uswisi.
Ingawa taarifa hiyo haikutaja majina ya watu wote
walioweka fedha Uswisi, imemtaja mfanyabiashara Shailesh Vithlani ambaye
anadaiwa kuwa dalali wakati Tanzania iliponunua rada kutoka kwa kampuni
ya BAE system kuwa ni miongoni mwao.Hivi karibuni, Waziri wa Fedha Saada Mkuya alikaririwa na baadhi ya
vyombo vya habari akitahadharisha kwamba si kila aliyeweka fedha Uswisi
amezipata kwa njia haramu.MWANANCHI
MWANASHERIA MKUU:
RIPOTI YA MABILIONI YA USWIZI IPO TAYARI
Na Lilian Timbuka, Mwananchi
Dar es Salaam. Kamati iliyoundwa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa
Serikali (AG), kuchunguza mabilioni ya fedha yaliyofichwa na baadhi ya
Watanzania katika benki mbalimbali nchini Uswisi, imekamilisha uchunguzi
na inasubiri kukabidhi ripoti ya kazi hiyo kwa Spika wa Bunge.
Hayo yalisemwa jana na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju
alipokuwa akizungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari, Dar
es Salaam.
Masaju alisema kamati hiyo ilikamilisha kazi yake baada ya kuwahoji watu
mbalimbali na kukamilisha kazi hiyo kama walivyoagizwa na Bunge na
kinachosubiriwa ni kuikabidhi kwa chombo hicho cha kutunga sheria.
“Ofisi yangu kupitia kamati iliyoundwa tulikwishamaliza kazi hii, lakini
hatuwezi kutoa taarifa kupitia sehemu nyingine zaidi ya ofisi
iliyotupatia kazi kama utaratibu unavyoelekeza.
“Sasa wananchi na nyie waandishi wa habari msubiri taarifa hiyo itolewe
kule bungeni ambako tuhuma hizi zilianzia,” alisema Masaju.
Watuhumiwa
Vigogo 10 wametajwa kuhusika katika kashfa hiyo. Inadaiwa kuwa katika
orodha hiyo, yupo kiongozi mmoja mwandamizi mstaafu, maofisa watatu
wastaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), mawaziri wastaafu
ambao baadhi yao bado ni wabunge na aliyewahi kuwa kiongozi mwandamizi
wa Benki Kuu Tanzania (BoT).
Kamati ilivyoundwa
Kamati hiyo maalumu iliundwa kwa Azimio la Bunge baada ya Mbunge wa
Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe kuibua tena tuhuma hizo bungeni mapema
mwaka jana, akidai kuna vigogo walioficha Sh323.4 bilioni katika benki
mbalimbali za Uswisi.
Kiasi hicho cha fedha kinaweza kujenga barabara ya lami yenye urefu wa
kilomita 300 ambao ni sawa na kutoka Morogoro hadi Iringa.
Kwa mara ya kwanza, tuhuma hizo zilitolewa bungeni na Zitto ambaye pia
ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), mwaka
2012.
Katika kikao cha Tisa cha Bunge, Zitto aliwasilisha hoja binafsi
kulitaka Bunge kuchunguza na kuielekeza Serikali kuchukua hatua dhidi ya
Watanzania aliowaita vigogo walioficha fedha na mali haramu nje ya
nchi.
Kutokana na hoja hiyo, Bunge chini ya Spika Anne Makinda, liliipa
Serikali muda wa mwaka mmoja ambao ulimalizika Oktoba mwaka jana iwe
imekamilisha uchunguzi na kuwasilisha ripoti yake bungeni.
Wakati sakata hilo lilipokuwa limepamba moto, Serikali ya Uswisi kupitia
kwa Balozi wake nchini, Olivier Chave iliwahi kusema Serikali ya
Tanzania haijaonyesha nia ya dhati kutaka kuchunguza na kurejesha
mabilioni ya fedha hizo.
Balozi Chave alikaririwa wakati huo akisema hawajaona jitihada zozote
zilizofanywa na Serikali ya Tanzania kutaka kuzipatia ufumbuzi tuhuma
hizo.
Chave alisema nchi yake iko tayari kushirikiana na Tanzania kujua
uhalali wa fedha hizo na endapo zitagundulika ni chafu watakuwa tayari
kuzirejesha nchini.
Taarifa kutoka Benki Kuu ya Uswisi inaonyesha kuwa baadhi ya fedha hizo
zimewekwa katika akaunti za vigogo hao na kampuni za mafuta na gesi
zilizopo nchini.
Hata hivyo, Machi mwaka jana ilielezwa kuwa mabilioni ya shilingi
yaliyowekwa na Watanzania katika benki za Uswisi yalikuwa yameanza
kuhamishwa kimyakimya.
Ripoti ya Benki za Uswisi ya 2012 ilionyesha kuwa fedha zinazotoka
Tanzania zilipungua kwa karibu Sh36.4 bilioni ikilinganishwa na
zilizokuwapo 2011 nchini humo, lakini haielezi sababu ya kupungua kwake.
Watanzania 99
Hivi karibuni, Timu ya Wanahabari wa Kimataifa wanaoandika Habari za
Uchunguzi (ICIJ) ilitoa ripoti ikisema Watanzania 99 wanamiliki Dola za
Marekani 114 milioni (Sh193bilioni) kwenye akaunti za benki nchini
Uswisi.
Ripoti hiyo inayoitwa SwissLeaks iliyotolewa Marekani, imesheheni
taarifa za Benki ya HSBC ya Uswisi na namna watu maarufu wakiwamo
wanasiasa, wachezaji, viongozi wa dini na wafanyabiashara walivyoficha
mamilioni ya fedha na kufanikiwa kuzikwepa mamlaka za mapato katika nchi
zao.
Katika orodha hiyo, Tanzania inashika nafasi ya 100 duniani na nafasi ya
pili Afrika Mashariki ikiwa nyuma ya Kenya inayoshika nafasi ya 58
duniani kwa kuweka zaidi ya Sh950 bilioni nchini Uswisi.
Ingawa taarifa hiyo haikutaja majina ya watu wote walioweka fedha
Uswisi, imemtaja mfanyabiashara Shailesh Vithlani ambaye anadaiwa kuwa
dalali wakati Tanzania iliponunua rada kutoka kwa kampuni ya BAE system
kuwa ni miongoni mwao.
Hivi karibuni, Waziri wa Fedha Saada Mkuya alikaririwa na baadhi ya
vyombo vya habari akitahadharisha kwamba si kila aliyeweka fedha Uswisi
amezipata kwa njia haramu.
MWANANCHI
Copy and WIN : http://bit.ly/copynwin
Copy and WIN : http://bit.ly/copynwin
Post a Comment