Mlinzi wa Chelsea Gary Cahill mwenye jezi ya
njano akikabiliana na mshambuliaji wa Paris Saint Germain ya Ufaransa
Zlatan Ibrahimovic. Timu hizo zilifungana 1-1
Michezo
ya ligi ya mabingwa barani Ulaya, UEFA ilianza kutimua tena vumbi
Jumanne usiku kwa michezo miwili katika hatua ya kumi na sita bora.
Paris
Saint Germain ya Ufaransa iliwaalika Chelsea ya England, huku Bayern
Munich ya Ujerumani wakiwa wageni wa Shaktar Donetsk ya Ukraine. Matokeo
ni kwamba PSG na Chelsea zimemaliza dakika tisini za mchezo kwa
kufungana bao 1-1.
Chelsea ndio waliokuwa wa kwanza kutikisa nyavu
za wenyeji wao katika dakika ya 36, bao likifungwa na Branislav
Ivanovic na kudumu hadi mapumziko. PSG waliendeleza mashambulizi huku
kiungo wake David Luiz akiwadhibiti wachezaji wa timu yake ya zamani,
Chelsea. Kwa David Luiz kutawala sehemu ya kiungo, mshambuliaji Matuidi
wa PSG alikuwa akitamba na kuelekeza mashambulizi makali langoni mwa
Chelsea na kumfanya mlinda mlango wake Curtois kuokoa michomo mingi.
Katika dakika ya 54 ya mchezo, Edinson Cavani aliisawazishia timu yake
bao na hivyo hadi mwamuzi anapuliza filimbi yake ya mwisho, timu hizo
zilitoka sare ya bao1-1. Bayern Munich ya Ujerumani katika mchezo wa
kwanza wa hatua ya 16 bora walipomenyana na Shakhtar Donetsk na kutoka
sare ya 0-0Nayo Bayern Munich ya Ujerumani ilishuhudia ikitoka sare ya kutofungana na Shakhtar Donetsk ya Ukraine.
Bayern Munich ilipata pigo kwa mchezaji wake Xabi Alonso kuzawadiwa kadi nyekundu katika mchezo uliojaa ubabe.
Jumatano
usiku, Real Madrid ya Hispania watakuwa wageni wa Schalke 04 ya
Ujerumani katika mchezo mwingine wa klabu bingwa, huku Basel ya Uswis
ikiikaribisha FC Porto ya Ureno.
Mechi za hatua ya kumi na sita bora zitakamilika Machi 18, ambapo michezo miwili miwili itakuwa ikifanyika Jumanne na Jumatano.
Timu
nyingine katika hatua hii ni Juventus ya Italia itakayopambana na
Borussia Dortmund ya Ujerumani, Manchester City ya England itavaana na
Barcelona ya Hispania, mechi zitakazochezwa usiku wa tarehe 24 Februari
na kesho yake yaani tarehe 25 Februari Arsenal ya England itakuwa
ikipimana misuli na Monaco ya Ufaransa, huku Bayern Levkusen ya
Ujerumani wakiwa wenyeji wa Atletico Madrid ya Hispania.
Post a Comment