0

Wabunge wa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo wamekubali mswada ambao wadadisi wanasema unakusudiwa kumpa Rais Joseph Kabila idhini ya kubaki madarakani, baada muhula wake wa pili kumalizika.
Mswada huo unapendekeza kufanywe sensa ya taifa kabla ya uchaguzi ambayo serikali inasema inaweza kuchukua miaka kadha kukamilisha.
Rais Kabila anamaliza muhula wa pili mwaka ujao.
Katiba ya nchi haimruhusu kugombea muhula wa tatu. wabunge wengi wa upinzani walisusia kura hiyo ya bunge, na kuielezea kuwa mapinduzi ya katiba.HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Post a Comment

 
Top