0
                                                   
Tume ya Taifa ya uchaguzi (NEC) inatarajia kutumia Bilion 293 kwa ajiri ya uboreshaji wa daftari  la wapiga kura ya maoni ya katiba mpya na uchaguzi mkuu mwezi oktoba mwaka huu ikiwa ni lengo la kukuza demokrasia hapa nchini.Haya ameyasema mwenyekiti wa tume ya Taifa ya uchaguzi Jaji Damian Lubuva alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya tume hiyo ya uchaguzi jijini Dar es salaam Jana.

Lubuva alisema kuwa suala la kuwepo wanajeshi katika uchaguzi wataangalia jinsi gani ya kufanya na kazi ya ulinzi ibaki mikononi mwa jeshi la oolisi.

Aidha alisema uandikishaji wa majaribio utambuzi wa alama ya mpiga kura kwa kifaa cha BVR ulikwenda vizuri na mapungufu yajitokeza na wataendelea kuboresha ili kila mtanzania mwenye sifa au kigezo aweze kujiandikisha na kuweza kupiga kura.


Post a Comment

 
Top