huyu ni mwingine askari alieuwawa katika tukio hili
Majambazi yaliyojihamu kwa silaha yamevamia Kituo cha Polisi cha
Ikwiriri, Rufiji mkoani Pwani na kuua askari wawili na kupora silaha
zilizokuwepo kituoni hapo.
Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia jana, huku askari wanaodaiwa
kupotenza maisha ni Cop. Edgar aliyekatwa mapanga na WP Judith
aliyepigwa risasi ubavuni upande wa kulia na kutokea upande wa kushoto.
Hivi sasa hali ni tete katika eneo hilo na watu wamekusanyika huku
polisi wakiongeza nguvu kusaka wauaji katika tukio la uvamizi, kituo cha
polisi Ikwiriri, Rufiji, Pwani.
Silaha zilizoporwa ni SMG 2, SAR 2, SHORTGUN 1, silaha 2 za mabomu ya machozi na risasi 60 za SMG.
Post a Comment