Ikulu imeitisha mkutano wa ghafla na
waandishi wa habari muda huu na mkutano huo utaanza ndani ya nusu saa
kuanzia sasa. Hii sio tetesi bali ni kweli.
Tetesi ni kwamba
mkutano huu umeitishwa ili kutangaza mabadiliko madogo ya mawaziri na
mawaziri hawa wanapaswa kuapishwa kesho kabla ya Rais Kikwete kuondoka
kwenda Davos Uswisi kesho hiyohiyo jioni.
Mabadiliko hatimaye yametimia. Nayo ni:
Mawaziri Kamili
George Simbachawene- Waziri wa Nishati na Madini
Mary Nagu -Waziri wa nchi Mahusiano na Uratibu
Harrison Mwakyembe - Waziri wa Afrika Mashariki.
Wiliam Lukuvi - Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi
Steven Wassira - Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika
Samwel Sitta - Waziri wa Uchukuzi
Jenista Mhagama - Waziri wa Sera na Uratibu wa Bunge
Christopher Chiza- Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji
Manaibu Waziri
Steven Masele - Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano
Angellah Kairuki - Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi
Ummy Mwalimu- Naibu Waziri wa Katiba na Sheria
Anna Kilango- Naibu waziri wa Elimu
Charles Mwijage - Naibu Waziri wa Nishati na Madini.
Post a Comment