MWAANDISHI WETU Nachingwea
,Chama cha Mapinduzi katika uchaguzi
uliofanyika kimefanikiwa kushinda vijiji
100 sawa na asilimia 80.64 kati ya vijiji 124 vilivyofanya uchaguzi huo ambao kwa baadhi ya maeneo yaligubika na vurugu
ambapo vijiji vitatu havikufanya uchaguzi.
Kwa mujibu
wa msimamizi wa uchaguzi wa halmashauri ya wilaya ya Nachingwea,Boniface
Chatila,alisema kuwa Chadema imenyakuwa
vijiji 12 sawa na asilimia 9.68 ,Cuf imeweza kupata vijiji 12 sawa
na asilimia 9.68.
Kwa upande
wa vitongoji Msimamizi huyo alisema kuwa
CCM imeshinda vitongoji 405 sawa na
asilimia 79.72 kati ya vitongoji 526 ambapo vitongoji 18 havikufanya uchaguzi
huo,Chadema imeshinda vitongoji 51 sawa
na asilimia 10.04 Cuf imeshinda
vitongoji 51 sawa na asilimia 10.04 na ADC ikiambulia kitongoji kimoja sawa na
asilimia 0.2.
Chatila alitaja
sababu ya vijiji na vitongoji hivyo kutofanya uchaguzi kuwa ni pamoja kukosekana kwa karatasi za
kupigia kura,makosa ya uchapaji kwenye karatasi za kupigia kura na kuwa
vijiji na vitongoji hivyo vinaendelea
kufanya uchaguzi huo na kuwa hadi
kufikia mwishoni mwa wiki hii maeneo yote yatakuwa yameshafanya uchaguzi.
“Maeneo
yasiyofanya uchaguzi ilitokana na makosa ya uchapaji kwani baadhi yalichanganya majina ya wagombea
“alisema Chatila.
Akizungumzia juu ya uchaguzi huo mwenyekiti wa Chadema
wilaya ya Nachingwea.
Post a Comment