0

Shirika la uchunguzi la mazingira lililo na makao yake nchini Uingereza, limesema wanadiplomasia na maafisa wa jeshi kutoka China, walinunua pembe haramu za ndovu walipokuwa katika ziara rasmi nchini Tanzania mwezi Marchi mwaka 2013. Maelfu ya tembo wanasemekana kuuwawa kila mwaka ili kukidhia mahitaji ya soko la bidhaa hiyo haramu katika mataifa ya Asia. Hata hivyo serikali ya Tanzania kupitia Mkurugenzi wa idara ya habari na maelezo Assah Mwambene imekanusha madai hayo na kusema kwamba ripoti iliyoelezea hayo iliotolewa hii leo ina lenga kuiharibia sifa Tanzania na kuharibu uhusiano mzuri wa nchi hiyo na China.DW

Post a Comment

 
Top