Mwenyekiti
wa Chama cha UPDP na aliyekuwa mbunge wa bunge maalum la katiba Mh.
Fahmi Dovutwa akitoa taarifa ya ushirikiano wa Vyama sita vya siasa
visivyokuwa na wambunge katika uchaguzi wa Serkali za Mitaa, Wabunge na
Rais unaotarajiwa kuanza mwishoni mwa mwaka huu mpaka mwaka 2015 ambapo
uchaguzi wa Wabunge na Rais utafanyika.
“Dovutwa
amesema vyama hivyo vimeamua kushirikiana kwa sababu vipo vyama
vilivyounda kundi lisilokuwa la kisheria linaitwa Ukawa, lakini hakuna
sheria inayoturuhusu kuunganisha vyama ila tunaweza kushirikiana tu
ndiyo maana tunasema tumekubaliana kushirikiana”. vyama vilivyokubaliana
kushirikiana ni SAUT, DEMOKRASIA MAKINI, JAHAZI ASILIA, UMD, UMD, UPDP
NA AFP , Katika picha wanaofuatia ni Dominic Lyamchai Mwenyekiti wa
Chama cha Demokrasia Makini, Rashid Lai Katibu Mkuu AFP na baadhi ya
viongozi wa vyama vya siasa.
Mwenyekiti wa Chama cha SAUT Yusuf Manyanga akifungua mkutano huo kabla ya Mwenyekiti wa UPDP Mh. Fahmi Dovutwa kutoa tamko.
Rashid Lai Katibu Mkuu AFP akifafanua
jambo wakati wa mkutano huo uliofanyika Sinza jijini Dar es salaam
kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha SAUT Yusuf Manyanga ,
Mwenyekiti wa UPDP Mh. Fahmi Dovutwa na Dominic Lyamchai Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia Makini.
Post a Comment