0
 
Rais Barack Obama (kulia) baada ya kumteuwa Loretta Lynch (kushoto) kuwa mwanasheria mkuu mpya, White House, November 8, 2014. 


Rais wa Marekani Barack Obama Jumamosi amemteuwa Loretta Lynch ambaye ni mwendesha mashtaka mkuu wa serikali New York, kuwa mwanasheria mkuu mpya Marekani.

Endapo ataidhinishwa na baraza la Senate, Lynch atachukua nafasi ya mwanasheria mkuu anayeondoka Eric Holder na kuwa M’marekani wa kwanza mwanamke mweusi kushika wadhifa huo.

Hadi uteuzi huo, Lynch alikuwa mwendesha mashtaka mkuu wa serikali ya Marekani huko Brooklyn New York.

Awali, msemaji wa White House Josh Earnest alisema Bi Lynch mwenye umri wa miaka 55, alisomea uwanasheria katika chuo kikuu cha Harvard na ana uzoefu wa kazi kama mwendesha mashtaka wa kibinafsi, aliyeongoza mojawapo ya ofisi muhimu za mkuu wa sheria nchini Marekani.

Post a Comment

 
Top