0
Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania
Rais wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete alifanyiwa upasuaji wa tezi dume (prostrate) katika Hospitali ya Johns Hopkins iliyoko Baltimore, Jimbo la Maryland nchini Marekani.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu ya Tanzania, Rais Kikwete amefanyiwa upasuaji huo baada ya madaktari waliomfanyia uchunguzi wa afya yake kujiridhisha kuwa Rais alikuwa anahitaji matibabu ya aina hiyo.
Upasuaji huo ulikuchukua kiasi cha saa moja unusu ambapo inaelezwa kuwa umefanyika salama na kwa mafanikio makubwa.
Taarifa hiyo inasema hali ya Rais Kikwete inaendelea vizuri japo bado yuko wodini akiendelea kuwa chini ya uangalizi wa madaktari na kupatiwa tiba.

Post a Comment

 
Top