0


               Mkuu wa wilaya ya Liwale Mh.Ephraim mmbaga|picha kutoka makitaba


 Mkuu wa wilaya ya liwale mh.Ephraim Mmbaga amemtaka kila kiongozi wilayani hapa awe wa chama au wa serikali kujiuliza amefanya nini kumuunga mkono mheshimiwa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania mh. Dr.Jakaya Mrisho Kikwete katika juhudi zake za kuhakikisha kuwa shule zote za sekondari nchini kote zina maabara.

Mkuu wa wilaya ametoa wito huo katika ziara yake ya siku tatu katika shule zote za sekondari zilizopo wilayani hapa kuanzia tarehe 28/10/2014 hadi tarehe 30/10/2014 lengo la ziara hiyo ni kukagua ujenzi wa maabara ambapo  kila jengo moja la maabara linatakiwa liwe na chumba tatu.

Akiongea na mtandao huu mara baada ya kumaliza ziara yake alisema"Jumla ya mahitaji yote ni vyumba vya maabara kwa shule 16 ni 48,vyumba vilivyopo kwenye hatua ya ukamilishaji ni 30 na kuna upungufu wa vyumba 18 pia aliendelea kusema kuwa jumla ya shilingi 950,000,000/= zinahitajika kugharimu zoezi hili muhimu kwa elimu na maandalizi ya wahitimu wanaoweza kuhimili ushindani  katika soko la ajira."  Shule zilizoanza utekelezaji wa ujenzi huo ni shule ya sekondari Nicodemus Banduka iliyopo katika kata ya Mbaya ambapo ujenzi wake umekamilika tayari na baadhi za shule zingine ujenzi wake unaendelea.Hizi ni baadhi ya shule za sekondari  zilizopo hapa wilayani kama LIWALE DAY,R.M KAWAWA,ANNA MAGOA,ANGAI,BARIKIWA,KIANGARA,NANGANDO,KIKULYUNGU,MAKATA,NANGANO.
   
 Mkakati huu wa mheshimiwa rais wetu umekuja kufuatia Taifa Kuwa na uhitaji mkubwa wa wanasayansi ili kwenda sambamba na ulimwengu suala ambalo kwa kipindi kirefu limekuwa likikwamishwa na ukosefu ama upungufu wa maabara katika shule zetu za sekondari.

Post a Comment

 
Top