0

Mwaandishi wetu Lindi....
Chama cha mapinduzi  kimesema kuwa  kashfa ya Escol  kila  mtu atachukua  msala wake mwenyewe  akiweza kuwavumilia viongozi  na watendaji wenye nia  mbaya  na serikali ya chama hicho  kwa kushindwa kusimamia  madaili, Demokrasia uadilifu, uwazi , uzalendo na  uwajibikaji .
Kauli hiyo imetolewa na katibu uenezi na itikadi taifa chama cha  mapinduzi Nape  Nnauye wakati alipokuwa anazungumza kwenye mkutano wa hadhara Lindi mjini ulifanyika uwanja wa Ilulu jana.
Nnauye alisema  kuwa muasisi wa maadili  na miiko ya uongozi wa umma  hapa nchini ni  chama cha mapinduzi  kuanzia Tanu na ndiyo sababu ya uunda azimio la arusha  na kuweka maadili ya uongozi ili kutekeleza  na kusimimia kwa vitendo dhana hiyo ya  maadili na miiko ya uongozi.
Alisema wapinzani hapa nchini wanasema kuwa chama cha mapinduzi kimepiga  na kuondoa kipengele za maadili ya umma kwenye katiba mpya iliyo pendekezwa  kwa kuwa itawabana viongozi walioko madarakani na kushindwa kufanya mambo yao watakavyo.
Nnauye  alisema kuwa chama cha mapinduzi kitaelendelea kusimamia maadili bila woga kwa kuwa shughulikia watu wote wenye nia mbaya nchi ndiyo maana kuna matuki mbalimbali yakiwemo sakata la Richmond lilopelekea waziri mkuu kujiuzuru chama kilichukumua maamuzi magumu na mazito ya kuwawajibisha waliohusika na matukio hayo.
“msimamo wa ccm juu ya maadili haujabadili uko palepale sikilizeni sikendo zote hata hii ya juzi  ccm itaendelea kusimamia maadili na ukishindwa  beba msalaba wako  tuachie ccm yetu salama” Alisema Nape
Kwa upande wake katibu wa ccm taifa Abrahamani Kinana alisema wakati wa kuomba ridhaa kwa wananchi  wagombea nafsi za  madiwani, wabunge  na urais kupitia  chama cha mapinduzi  muda wa waliahidi  mambo  mengi  hivyo basi ni wajibu wa chama kurudi kuangalia utekelezaji wa mambo yote yaliyohaidiwa ili kuhimiza pale inapolegalega.
Kinana alisema muda  kuvumiliana ,kubebana  na kulinda umeisha kwani imekuwa tabia na ugonjwa kwa baadhi ya vingozi kushindwa kusimamia  na kukosoa punde watendaji wanaposhindwa kuwajibika ipasavyo , chama cha mapinduzi hakiwezi kuvumbia macho mwenendo huyo ambao  unasababisha wananchi kukosa imani na chama.
“Kazi ya ccm ni kusimamia utekelezaji wa ilani yake hakiwezi kusifia kila jambo hata likiwa la hovyo  hatuwezi kusifia kila kitu kienda vizuri tutasifia kikienda vibaya tutasema na kukosoa wakiendeleza zaidi tutashikana masharti “alisema Kinana

Post a Comment

 
Top