0
Kamanda mwingine wa Burkinafaso amejitangaza kuwa rais wa muda wa Burkinafaso baada ya Rais Blaise Compaore wa nchi hiyo kulazimika kujiuzulu na hivyo kuwa kamanda wa pili kujitangaza kuwa rais wa Burkinafaso.
 
Kanali Yacouba Isaac Zida ametangaza uamuzi wa kushikilia kiti cha urais wa mpito huko Burkinafaso kupitia hotuba aliyoitoa na kutumwa leo asubuhi katika tovuti ya kituo cha taifa cha televisheni ya nchi hiyo.
Zida kamanda wa zamani wa kikosi cha ulinzi wa rais amesema kuwa amechukua uamuzi wa kujitangaza kuwa rais wa mpito wa Burkinafaso kutokana na uungaji mkono mdogo alionao Jenerali Honore Traore Mkuu wa majeshi ya nchi hiyo.
 
Kanali Yacouba Isaac Zida ameyasema hayo hii leo masaa machache baada ya Jenerali Traore kutangaza kuchukua nafasi ya rais huko Burkinafaso

Post a Comment

 
Top