WAFUGAJI WAINGIA ndani ya msitu wa hifadhi Nyera Kipelele wilayani Liwale mkoani Lindi kuendesha malisho
MBUNGE
APORA ARDHI YA WANANCHI.
Na mwaandishi wet liwale.
Liwale.Wananchi
wa Kijiji cha Kibutuka wilaya ya Liwale,mkoa wa Lindi wanalalamikia kitendo cha
Mbunge wao,Faith Mohamed Mtambo kumilikishwa eneo lenye madini aina ya Manganise bila
kufuata taratibu zilizoainishwa na sheria ya ardhi namba 5,1999 na sheria ya
Madini ya mwaka 2010 pamoja na Sera zake hivyo kusababisha mgogoro kati ya wanakijiji
na mbunge huyo.
Akizungumzia
Mgogoro huo, mkazi wa kijiji cha Kibutuka, Chande Majate alisema wananchi wa kijiji hicho wamestushwa na
kitendo cha Mbunge huyo kumilikishwa
eneo hilo tangu mwaka 2011 bila wao kushirikishwa, na kuwa hawajui ametumia taratibu gani za kisheria kumiliki
eneo ambalo wamiliki halali na serikali
ya kijiji.
Alisema
kuwa eneo hilo ambalo iwapo litachimbwa kwa kutumia mitambo ya kisasa linaweza
kufanya kazi kwa muda wa zaidi ya miaka ishirini na tano lina madini ya aina ya Manganise ambayo yanatumika
kama urembo majumbani na pia kuna aina
nyingine saba za madini ikiwemo dhahabu, shaba na mengine.
Alibainisha
kuwa eneo hilo liligunduliwa na wenzao wawili wa kijiji hicho, Abdul Kujakila
na Hemedi Majate baada ya kuyaona mawe
ndipo waliyachukua na kumtafuta mtu mwenye
uzoefu na masuala ya madini
ambaye aliwajulisha kuwa mawe hayo ambayo pia yameenea katika maeneo mengi kwenye kijiji
hicho na vijiji jirani ni madini ya manganise.
Alisema
kuwa baada ya ugunduzi huo serikali ya kijiji
baada kupata baraka ya mkutano wa kijiji ilimpa kibali Faridi Mpili ili
aanze mchakato wa kupata hati miliki ya eneo hilo ambalo lina ukubwa wa kilometa za
mraba 70 ili kuanza uchimbaji kwa sharti la kuingia ubia na wananchi wa kijiji
hicho wa kushirikisha wachimbaji wadogo wadogo.
Kwa upande wake,Ramadhani Kwepu,Mkazi wa
kijiji cha Kibutuka alionesha kushangazwa na mchakato mzima wa kumpatia hati
mbunge huyo kwani katika mchakato huo wananchi ambao ndio wenye mamlaka ya
kuridhia upatikanaji wa ardhi ya kijiji hicho hwakushirikishwa hali inayotia shaka kwa uwepo mazingira ya
rushwa .
Alisema
kuwa walishangaa kuwaona watu waliojiita
wawekezaji ambaye ni Francis Mutalemwa
na wenzake kwenye eneo hilo ambalo licha
ya kuwa katika kijiji cha Kibutuka linajumuisha na vijiji vya jirani ambavyo
hata uongozi wa vijiji vyao hauna
taarifa ya maeneo yao kumilikiwa na Mbunge huyo ambao
walianza kuchimba bila ya kufuata taratibu na kudai kuwa wao walitumwa na Faith
Mtambo jambo lilisababisha wananchi kuwatimua huku wakitelekeza madini yenye
uzito unaokadiriwa kuwa Tani mia tano,
Kwepu
ambaye ni mmoja kati ya wajumbe wanaofuatilia sakata hilo la umiliki wa Kampuni
iliyotambulika kwa jina la Linda Ruta company ambayo imebainika ni jina la
mmoja wa Mtoto wa Mbunge huyo, alibainisha kuwa licha ya kudai eneo hilo ambalo
pia linagusa maeneo ya vijiji vya
Kiangara,Mihumo,Nangano,Kipelele,Ngumbu na Kitogoro kumilikiwa na Mtoto wa
mbunge huyo, anayetoa maelezo na kutajwa ni Mbunge Mtambo badala ya Linda
ambaye inadaiwa kuwa ndiye anamiliki.
Alisema kuwa kutokana na uwepo wa mgogoro
huo kuna mawe yenye uzito wa Tani zipatazo
500 za madini ya manganasi yanashindwa kuondolewa ambayo yalivunjwa na
Mutalemwa na wenzake kufuatia kutimuliwa na kusitishwa na uongozi wa kijiji kwa
kushirikiana na wananchi.
Hamisi
Kichoti mkazi wa kijiji cha Kibutuka Alishangazwa na kauli ya Mbunge huyo kuwa anawafahamu
na kuwa atawataja wamiliki wengine wa vitalo
vingine kati ya vitalu 12 vilivyopo katika eneo hilo lakini hajawataja wamiliki hao hali inayotia
shaka kuwa uenda hata vitalu
vingine vinamikiwa na mbunge huyo.
"Kitendo
cha Mbunge huyo kusema kuwa anawajua wamiliki wa vitalu vingine inatia shaka
kuwa uenda vitalu vyote vinavimilikiwa yeye"alibainisha Kichoti.
Alisema mbunge huyo kama kweli anataka kumiliki eneo
hilo afuate tararatibu za kisheria kwa kupeleka maombi kwa serikali ya kijiji
ambapo ataeleza wananchi wapatao 7,890 wanaoishi kwenye maeneo hayo
watakavyopata fidia kutokana na eneo lao
kumikiwa, ambapo vijiji husika vitanufaika na nini kwa uwepo wa mgodi huo.
Mwenyekiti wa kijiji hicho, Rajabu Kwepu alikiri kuwa upo mgogoro huo
ambao alisema kuwa licha ya mbunge huyo kukiri na kuomba radhi kupitia mkutano
mkuu wa kijiji kuwa anamiliki bila kushirikisha wananchi na kuwa angekuja rasmi
kufafanua hoja hiyo lakini hajafika kijijini hapo.
Aidha
alibainisha kuwa wananchi walimtaka
awataje wamiliki wengine wa vitalu ambapo mbunge huyo alidai anawafahamu na
kuwa atawataja jambo ambalo hajalitekeleza hadi hivi sasa na hivyo
ametakiwa kutekeleza makubaliano hayo.
"Tulimwita
kwenye mkutano wa wananchi wote uliofanyika mwezi wa tatu mwaka huu u ili
awataje wamiliki wa vitalu vingine kama alivyoahidi hata hivyo hajalitekeleza
ahadi hiyo"alisema Kwepu.
Mwenyekiti
wa kijiji cha Mikunya,Saidi Mkongoteka,moja ya kijiji ambacho
limo eneo ambalo linamilikiwa alisema uongozi wake umepata taarifa zisizo rasmi
juu ya Mbunge kumiliki eneo kubwa ambalo kijiji chake kimo ndani ya eneo hilo
na kuwa kwa sasa wanafuatilia kuona
ukweli wa jambo hilo.
Alibainisha
kuwa iwapo ikibainika kuwa taarifa hizo ni za kweli Serikali ya kijiji hicho haitakubalia
hivyo kumtaka mbunge huyo kuacha kabisa eneo hilo na kuwa uenda ikachukua hatua
za kisheria za kisitisha umiliki huo.
"Kwa
sasa tunafuatilia ukweli wa taarifa hii kwa hatujaipata rasmi,hata hivyo
namtaka ndugu yangu(Mbunge) kuachana na eneo hili kwa tukibaini kuwa zinaukweli
hatutasita kumfikisha kwenye vyombo vya sheria ili kusitisha umiliki
wake"alisema Mkongoteka.
Naye,
Nasoro Pyandu mjumbe wa serikali ya kijiji cha Kitogoro ambacho nacho
kimekumbwa kwa eneo lake kuwa ndani ya eneo la mbunge huyo, alieleza kuwa
hawajapokea ombi lolote la kampuni au mwekezaji
la kutaka umilikiwa wa eneo hilo kwa lengo la kuchimba au kufanya utafiti wa
Madini na kuwa anayo taarifa ambazo si rasmi kuwa Mbunge anamiliki eneo kubwa
ambalo limeingia hadi kwenye kijiji chao.
Alisema
kuwa iwapo jambo hilo litakuwa na ukweli basi anaomba uongozi wa kijiji hicho
kuitisha mkutano wa kijiji ili ujadili kwa kina na kupata ufumbuzi na uamuzi wa pamoja kwani eneo hilo ni mali ya wananchi wa kijiji
hicho kisheria.
“Lisemwalo
uenda lipo hivyo Iwapo kuna ukweli au la juu ya umiliki huo, nadhani busara
ambayo nitawaomba viongozi wetu ni kuitisha mkutano wa wananchi wote ili watoe
uamuzi juu ya ardhi yao"alisema Pyandu.
Faridi
Mpili ambaye awali aliwabainishia wananchi hao kuwa mawe yaliyopo kwenye kijiji
hicho ni madini ya Manganise alisema baada ya kugundua kuwa eneo hilo lina
madini hayo uongozi na wananchi kupitia mkutano wa kijiji walimpa kibali cha
kuanza mchakato wa kupata hatimiliki na kuwa baada ya kuwasilisha barua hizo
ofisi ya Madini kanda ya kusini akakuta eneo hilo linamikiwa na Mbunge,Faith Mtambo
tangu 28/12/2011 akitumia kampuni iliyotambukika kwa jina la Linda Ruta
company.
Kwa upande
wake,Mkuu wa wilaya ya Liwale,Hephrem Mmbaga alikiri kuwepo kwa mgogoro
huo baada ya suala hilo kufikishwa mahamakani na Francis Mutalemwa na wenzake ambao walipinga kusimamishwa
shughuli za uchimbaji ambapo mkuu huyo alisema ofisi yake haina mamlaka ya
kuingilia masuala ya madini na kuwa uwezo wake ni kuhakikisha hakuna migogoro
kwa kutoa ushauri kwa Kamishna wa Madini.
"Jukumu
langu mimi kama Mkuu wa wilaya ni kutoa
ushauri kwa kamishna wa madini iwapo kunajitokeza stofahamu ... kwani hata
wanapofanya shughuli zao sheria haiwalazimishi kutoa taarifa kwangu na hii sisi
kama wakuu wa wilaya tumekuwa tukiipinga sana na kutaka hii shreia iangaliwe
upya"alisema Mmbaga.
Kamishna
wa Madini kanda ya Kusini
inazungumziaje.
Kamishna
wa madini kanda ya Kusini, Injinia Benjamini Mchwampaka, alisema kuwa hana taarifa ya mgogoro huo kwa kuwa ni
mgeni hivyo alisema ataitahitaji muda ili kuangalia kumbukumbu za ofisi kuona undani wake.
"Binafsi
mimi hapa ni mgeni kabisa ila ninachojua ni kuwa ofisi inatoa leseni kwa
Kampuni iliyokamilisha vigezo vya kisheria kwa hilo sina jibu la moja kwa moja
mpaka nifuatilie kumbukumbu zake"alisema Mchwampaka.
Naye
Aloisi Tesha, Kamishina wa madini ambaye hivi sasa amehama anayedaiwa
kushirikiana na Mbunge huyo kumikilisha eneo hilo alipotakiwa kutoa ufafanuzi
wa tuhuma hizo alikiri kutambua umiliki wa eneo hilo na kudai kuwa Mbunge huyo
alifuata taratibu zote za kisheria za umiliki wa eneo hilo na kuwa yeye alitoa
hati baada ya kuridhika kuwa amekidhi vigezo vilivyoaishwa na sheria ya Madini.
Mbunge
aelezea
Alipoulizwa
kuhusiana na malalalmiko ya wananchi hao,Mbunge wa jimbo la Liwale Faith Mtambo
alikiri kuwa ana eneo anamiliki ambalo lipo katika kijiji cha Kibutuka na kuwa amelipata kwa
kufuata taratibu za kisheria na kuwa uongozi wa kijiji hicho unatambua kuwa
anamiliki eneo hilo.
“Ni
kweli nina miliki eneo katika kijiji hicho lakini sijawahi kuwasiliana na
serikali ya kijiji wala kukutana na wananchi juu katika kupata uhalali bali
kamishna wa madini kanda ya Kusini na kuwa hivi sasa anatarajia kukutana na
uongozi wa kijiji hicho”alisema Mtambo na kupongeza kuwa"Mwenyekiti wa
kijiji uwa nawasiliana mara kwa mara nakuwa naratajia mwezi wa saba kukutana na
serikali ya kijiji baada ya kukamilisha taratibu zote kwa Kamishna wa madini"alisema
Mtambo.
Mbunge huyo alisema kuwa si shida yeye
kumiliki eneo kwenye kijiji hicho kwani naye ni mkazi wa Liwale na kuwa kuna
kuna vitalu vingine vipatavyo hamsini ambavyo vinamilikiwa na watu wanaoishi
nje ya Liwale na kuwa jukumu lake kama mbunge pia ni kuwatafutia hao wamikili
ambapo tayari ameshapata ramani na majina yao ambayo hatayawasilisha kwa
serikali ya kijiji ili wawafuatilie waliko na kupata kumbukumbu zao.
"Mimi
sioni kama kuna shida yoyote ya mimi
kuwa na kitalu kwenye kijiji hicho,… kwani nami pia ni mwana Liwale mbona kuna
vitalu vingine hamsini vinamilikiwa na watu tena kutoka nje ya Liwale lakini
hawaulizwi kwa nini mimi"alihoji Mbunge huyo.
Mbunge huyo alisema haoni kama ni dhambi kwa yeye kumiliki eneo
kwenye kijiji hicho na vijiji vingine ndani ya Liwale kwani naye ni mkazi wa
wilaya hiyo na kuwa kuna licha yake pia
vipo vitalu vingine vipatavyo hamsini
ambavyo vinamilikiwa na watu wanaoishi nje ya Liwale na kuwa jukumu lake pia ni
kuwatafutia hao wamikili ambapo tayari ameshapata ramani na majina yao ambayo
hatayawsilisha kwa serikali ya kijiji ili wawafuatilie waliko na kupata
kumbukumbu zao.
"Mimi
sioni kama kuna shida yoyote ya mimi
kuwa na kitalu kwenye kijiji hicho,… kwani nami pia ni mwana Liwale mbona kuna
vitalu vingine hamsini vinamilikiwa na watu tena kutoka nje ya Liwale lakini
hawaulizwi kwa nini mimi lakini nashangaa mimi kumiliki eneo imekuwa nongwa "alihoji
Mbunge huyo.
Alibainisha
kuwa licha ya yeye kumiliki maeneo hayo pia kuna watu wengine wapatao 50 ambao pia wanamiliki maeneo
hayo na kuwa kama Mbunge amefanya uchunguzi na kuwabaini na kuwa atawasiliana
na uongozi wa kijiji cha Kibutuka ili wawaite wamiliki hao ili waonesha
leseni zao na pia waeleze jinsi wananchi watakavyonufaika na
uwepo wao.
“Mimi
nakusudia kukutana na uongozi wa kijiji cha Kibutuka na vijiji vingine kwa
lengo kuwatajia watu wengine ambao wanamiliki maeneo hayo kwani ni moja kati ya
majukumu yangu kama mbunge wao,”alisema Mtambo.
Alisema kuwa tatizo hapo
si yeye kumiliki eneo kwenye kijiji
hicho kwani ana haki kwa kuwa ni mkazi
wa Liwale bali kikubwa ni namna gani wananchi
wa maeneo hayo jinsi watavyofaidika na uwepo wa madini hayo kwenye maeneo yao.
Sheria
ya ardhi inasemaje,
Kwa mujibu wa Sheria ya ardhi na 5, 1999, Serikali ya kijiji imeanishiwa kazi mbalimbali ambazo ni pamoja
na kupokea, kutafakari na kuamua au kupendekeza kwa mkutano mkuu wa kijiji
maombi ya ugawaji wa ardhi na rasilimali nyingine ya kijiji.
Aidha
Mkutano mkuu wa Kijiji katika sheria hiyo imeweka wazi kazi zake ambazo ni
Kupitisha au kukataa mapendekezo ya ugawaji wa ardhi kijijini, Kupitisha
wajumbe wa Baraza la Ardhi la Kijiji, Kupitisha au kukazia mapendekezo ya
wajumbe wa Kamati ya Ardhi Kijijini, Kupitisha au kukataa Mpango wa Maendeleo
ya Kijiji juu ya matumizi ya ardhi na Kupokea taarifa ya namna ardhi ya kijiji
inavyosimamiwa.
Kwenye
sheria hiyo pia imeanisha hatua za
kufuata ambazo mwekezaji anatakiwa kufuata ambapo sheria inamtaka Mwekezaji kuwasilisha
barua kijijini akielezea kiasi cha eneo analoliomba,na madhumuni ya matumizi ya
ardhi anayoiomba.
Halmashauri
ya Kijiji itajadili barua ya maombi na kuandika maoni yao,sababu za kukubali au
kukataa kumpa mwekezaji ardhi na kupeleka maoni yao kwenye Mkutano Mkuu wa
Kijiji.taarifa zinazohusiana na uhamishaji wa umiliki, pamoja na maelezo ya
ardhi, maelezo ya watu watakaoathirika(kama wale watakaopoteza ardhi, ambao
sasa wanamiliki kwa kufuata sheria za kimila)
Fidia
kwa kijiji na wale waathirika wa moja kwa moja na mafao yoyote yatakayopatikana
kijijini kwa sababu ya uwekezaji yanapaswa kubandikwa wazi sehemu zote, karibu
na eneo linaloombwa.
Sheria
ya Madini namba 14/2010 inasemaje.
Sheria
ya madini imeeleza wazi kwenye maeneo
mbalimbali ikiwemo na Maeneo maalum kwa leseni za awali ambapo kwenye Kifungu
cha 16 kinaainisha kuwa waziri baada ya kushauriwa na bodi akiona kwa maslahi
ya sekta nzima ya uchimbaji nchini Tanzania ataweza kutoa amri na kuchapisha
kwenye gazeti la serikali,Kutenga eneo lolote lililo wazi na kulitangaza eneo
lolote lililotengwa kwa wachimbaji wadogo kwamba limetengwa maalum kwa ajili ya
watu wenye leseni za uchimbaji za awali chini ya daraja D sehemu ya nne.
Sheria
hiyo pia inaweka Makatazo ya haki ya kuingia kwa mmiliki wa haki ya madini
ambapo kwa mujibu wa kifungu cha 95 mmiliki wa haki ya madini haruhusiwi
kutumia leseni aliyopewa kwa sheria hii kuingia kwenye eneo ambalo limetengwa
kwa shughuli nyingine mfano shughuli za kijamii, eneo la makaburi, eneo la
jeshi au eneo lolote la hifadhi mpaka apate kibali cha maandishi toka kwa
waziri husika.
Vilevile
mmiliki hataruhusiwa kutumia leseni hiyo na kuingia kwenye eneo bila
mashauriano na serikali za mitaa ikijumuisha halmashauri za vijiji na kibali
cha mmiliki halali wa eneo hilo. Pale ambapo Waziri anaona upatikanaji wa
kibali kinachotakiwa unacheleweshwa bila sababu Waziri husika anaweza kutoa
kibali hicho kana kwamba kimetolewa na mmiliki halali wa eneo hilo.
Kwenye
maeneo ambayo yanamilikiwa na mamlaka nyingine kama hifadhi za taifa, maeneo ya
reli, barabara au maeneo yaliyotolewa kwa shughuli maalum, mmiliki ataingia kwa
kibali kutoka kwa mamlaka au waziri husika.SAUTI YA KUSINI
Post a Comment