HONGERA MBUNGE FAITH MITAMBO kwa kusimikwa Ukamanda wa vijana wilaya Liwale ,Maneno ya Hasani mpako
Mwenyekiti wa ccm mkoa wa Lindi Mohamedi Mtopa akifafanua jambo kwenye mkutano wa uvccm wilaya Liwale mkoani Lindi
Na mwaandishi wetu Liwale,……
Wanachama wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM) wilayani Liwale Mkoa wa Lindi wamegawanyika makundi mawili na kusabisha uvutano na
vurugu ndani ya chama kwa kile
kinachodawai kuwa ni kambi za ubunge 2015
Hayo
yamebainishwa na baadhi ya waanachama
wakati walipokutana na timu ya waandishi wa habari waliotembelea wilayani humo
Akizungumza kwa niaba
ya wezake Mohamedi Mbamba alisema kuwa mbunge wa jimbo hilo Fairth Mitambo na mbunge wa viti maalumu Zainabu Kawawa ndiyo
chanjo cha migogoro hiyo inayosababisha kutoelewana na kujenga makundi ndani ya chama hicho.
Mbamba alisema
hali ya chama cha mapinduzi wilaya ya Liwale ni tete kutokana na kuwepo
kwa makundi yanayosababishwa na tamaa na
kujali maslai binafsi kwa baadhi ya wanachama na watendaji wa chama
hicho ngazi ya wilaya.
Aisha Nakajumwe
alisema mjumbe ambaye ni mjumbe wa mkutano mkuu UWT wilaya alisema vita kati ya
kundi la mbunge Faith Mitambo na Zainabu Kawawa ni kukombea jimbo kwani inadaiwa kuwa Zainabu Kawawa anania ya
kuomba ubunge Jimbo la Liwale
Aisha alisema kuwa
hali ya mvutano huyo unasababisha wanachama kugawanyika sambamba na mbunge Faith Mitambo kutozipa ushirikiano wa kutosha jumuia za
chama ikiwemo ya Wazazi,wanawake na vijana
kwa madai zinatumiwa na watu
wanaotaka kugombea ubunge jimboni humo
ili kumwangusha.
“Tabia ya mbunge
wetu sio mzuri sisi jumuia ya wazazi
tumeaanda mkutano wa baraza la wilaya la wazazi tulivyokwenda kwake kuomba mchango akatuambia
twende kwa mbunge wetu Zainabu Kawawa we kaka majibu hayo ya mbunge kweli ni busara” alihoji Aisha.
Alipoulizwa kuhusiana na madai hayo,Zainabu kawawa alisema
kuwa hakuna ubaya way eye kuomba ubunge
jimbo la Liwale ni haki yake ya msingi,
kuchagua au kuchaguliwa ila muda wa kutangaza nia bado haujafika.
Kawawa aliongeza kuwa
yeye ni mbunge wa viti maalumu mkoa wa Lindi
kwa hiyo ana haki ya kuwahudumia
wananchi wa jimbo yote waliyoko ndani ya mkoa huo,
Kwa upande wake mbunge
wa jimbo hilo,Faith mitambo alisema hawezi kuongelea mambo ya chama nje ya
vikao halali vya chama.
Hali hiyo inaashiria
kwamba juhudi za kumaliza mgogoro huyo
zilizofanya na kamati ya siasa ya Mkoa
imegonga mwamba ambapo kamati ya siasa ilikutana mwezi octoba wilayani humo kumaliza mpasuko wa chama ndani
ya wulaya hiy
kamanda wa vijana Liwale mjini faith mitambo akipongezwa na katibu mwenezi ccm mkoa wa LIndi Ibrahim Mpwapwa
Na mwaandishi wetu Liwale
Makamu mwenyekiti wa Taifa wa umoja wa vijana wa
CCM,Mboni Mhita amewahasa Makamanda wa
umoja wa vijana wa CCM nchini kuzisukuma
halmashauri kutoa fedha zilizotengwa na serikali kwa ajili ya vijana na
wanawake.
Hayo aliyaeleza wakati
wa sherehe za kumsimika kamanda wa
wilaya ya Liwale,Faith Mitambo iliyofanyika siku ya jumamosi ,ambapo alisema
kuwa bila msukumo wa makamanda hao bado vijana watakuwa wanaangaika kupata
mitaji wakati serikali inatenga fedha.
“Inahitajika msukumo wa
mara kwa mara kwani kumekuwa na tabia ya
baadhi ya halmashauri kutumia fedha hizo kwa shughuli zingine badala ya lengo
lililokusudiwa na serikali”alisema Mhita.
Alibanisha kuwa wao
kama walezi wa vijana wanalojukumu la kuwainua na kuwaendeleza vijana kiuchumi
na biashara ikiwa ni pamoja kuwasaidia wale wenye vipaji mbali hasa wanamuzi chipukizi ili wanufaike
na vipaji vyao.
Aidha amewataka vijana
wote hapa nchi kuacha kushinda vijiweni badala yake wajishughulishe katika shghuli za kiuchumi kwani suala la
siasa ni lazima liendane na uchumi.
Akizungumza kwenye
sherehe hizo ambazo pia zilizohudhuriwa na Naibu katibu mkuu wa umoja wa vijana
Taifa, Hasan Mpokwa, Kamanda wa vijana wa CCM wilaya ya Liwale ambaye pia ni
mbunge wa Liwale,Faith Mitambo aliahidi
kufuatilia fedha hizo ili
ziwanufaishe vijana kama ilivyokusudiwa.
MAKAMANDA wa vijana kata ya Liwale mjini na Nangando wilayani Liwale mkoani Lindi wa kwanza Mkoyage Liwale Mjini WAPILI Kutoka Kushoto Hasani Myao diwani kata ya Nangando
Post a Comment