Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), linatarajia kuendelea na awamu ya
pili ya maboresho ya timu ya Taifa (Taifa Stars) inayojumuisha vijana
wenye umri chini ya miaka miaka 23.
Katika awamu hii, Kocha wa Taifa Stars, Mart
Nooij ameteua majina ya wachezaji 29 ambao watakuwa wakiingia kambini
mara moja kwa mwezi siku ya Jumapili baada ya kuwakilisha timu zao
kwenye mechi za ligi.Kikosi hicho cha maboresho kitakuwa kikifanya
programu maalumu za mazoezi mpaka siku ya Jumatano na kucheza mechi za
kirafiki na timu za ndani au nje ya nchi.Lengo hasa la programu hiyo ni
kuwajengea uwezo vijana wenye vipaji ambao walipatikana katika awamu ya
kwanza ya mpango wa maboresho mwanzoni mwa mwaka huu Tukuyu mkoani
Mbeya, lakini wamekuwa hawatumiki. Pia kuwandaa vijana ili kujenga timu
ya ushindani na imara ya Taifa ya muda mrefu.
TFF ina
imani kubwa kuwa programu hii itakuwa na manufaa kwa soka ya Tanzania.
Timu hiyo itaingia kambini kwa mara ya kwanza Desemba 9 mwaka huu katika
hoteli itakayotangazwa baadaye.
Wachezaji
walioteuliwa ni Aishi manula (Azam), Benedict Tinoco (Kagera Sugar),
Aboubakar Ally (Coastal Union), Miraji Adam (Simba), Andrew Vicent
(Mtibwa Sugar), Gadiel Mbaga (Azam), Emmanuel Semwanda (African Lyon) na
Joram Mgeveke (Simba).
Edward
Charles (Yanga), Hassan Mwasapili (Mbeya City), Kassim Simbaulanga
(African Lyon), Pato Ngonyani (Yanga), Adam Salamba (Kahama), Hassan
Banda (Simba), Mohamed Hussein (Simba), Hashim Magoma (Stand United),
Makarani Ally (Mtibwa Sugar), Said Juma (Yanga) na Said Hamis (Simba).
Aboubakary
Ally Mohamed (Zanzibar), Hassan Dilunga (Yanga), Hussein Malombe (Geita
Gold), Muzamir Ally (Mtibwa Sugar), Shiza Ramadhan (Mtibwa Sugar),
Omari Nyenje (Ndanda SC), Kelvin Friday (Azam), Salim Mbonde (Mtibwa
Sugar), Alfred Masumbakenda (Kahama) na Simon Msuva (Yanga).
Post a Comment