MTU
MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA YASSINI HEZRON (14) MKAZI WA KIWIRA
ALIFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.235 AFB
AINA YA M/CANTER LILILOKUWA LIMEBEBA MATOFALI LIKIENDESHWA NA DEREVA
AITWAYE FREDY MPONDO KUSHINDWA KUPANDA MLIMA NA KISHA KURUDI NYUMA NA
KUANGUSHA MATOFALI NA KUSABABISHA KIFO KWA TINGO HUYO.
AJALI
HIYO IMETOKEA MNAMO TAREHE 29.10.2014 MAJIRA YA SAA 12:00 MCHANA HUKO
MAENEO YA NEW LAND BAR, KATA YA KIWIRA, TARAFA YA UKUKWE, WILAYA YA
RUNGWE, MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA YA TUKUYU/KYELA. CHANZO CHA AJALI
NI GARI HILO KUSHINDWA KUPANDA MLIMA NA KURUDI NYUMA. MWILI WA MAREHEMU
UMEFANYIWA UCHUNGUZI NA KUKABIDHIWA NDUGU KWA MAZISHI. DEREVA ALIKIMBIA
MARA BAADA YA TUKIO HILO NA JUHUDI ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED
Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA NA WATUMIAJI WENGINE WA VYOMBO VYA
MOTO KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO HIVYO IKIWA NI PAMOJA NA KUZINGATIA
SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOEPUKIKA.
AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA
[DEREVA] KUZITOA KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA
ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.
TAARIFA ZA MISAKO:
JESHI
LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WANNE WALIOFAHAMIKA KWA
MAJINA YA 1. OTHAZ ANGOLILE (18) 2. SAMSON MWANGOMILE (46) 3. FORD
SAMSON (20) NA 4. BARAKA JOSEPH (23) WOTE WAKAZI WA AIRPORT JIJINI MBEYA
WAKIWA NA POMBE KALI ZILIZOPIGWA MARUFUKU NCHINI AINA YA BOSS NA RIDDER
PAKETI 108.
WATUHUMIWA
WALIKAMATWA KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA MNAMO TAREHE 29.10.2014 MAJIRA YA
SAA 11:00 ASUBUHI HUKO KATIKA MTAA WA AIRPORT, KATA YA IYELA, TARAFA YA
IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. WATUHUMIWA NI WAUZAJI WA POMBE HIZO NA
TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED
Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA/KUUZA POMBE KALI
ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA SERIKALI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI
HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Post a Comment