Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa
Mataifa, Wanawake, Anna Collins akitoa hotuba yake wakati akifungua
warsha ya siku moja kuhusu Malengo ya Milenia kwa washiriki mbalimbali
na kwa kiasi ngani Tanzania imeweza kufikia malengo hayo.iliofanyika
Makao Makuu ya Taasisi ya Uchumi na Utafiti wa Kijamii nchini (ESRF)
Oktoba 27, 2014 jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi wetu
SERIKALI ya Tanzania imekataa rasmi
kutambua ndoa za jinsia moja (ushoga) kama moja ya agenda za maendeleo
katika malengo ya milenia 2015 mpaka 2030 katika mkutano wa Umoja wa
Mataifa.
Akizungumza jijini Dar es Salaam
kwenye mkutano wa majadiliano ya malengo ya milenia yanayotazamiwa
kumalizika mwakani na kuanza malengo mapya, Mkurugenzi wa Idara ya
Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy amesema serikali ya
Tanzania imekataa kutambua ushoga kama moja ya agenda za maendeleo.
“tunatambua haki za binadamu, usawa
wa kijinsia kati ya wanaume na wanawake na hata katiba yetu pendekezwa
imetoa haki za sawa kati ya wanaume na wanawake lakini katika swala la
kutambua ndoa za jinsia moja hilo tumekataa,” amesema Balozi Mushy
Amesema kwamba tumewaambia nchi
zilizoendelea na wahisani wa maendeleo katika Umoja wa Mataifa kwamba
swala la ndoa za jinsia moja (ushoga) si agenda ya watanzania na si
agenda ya maendeleo.
Mkurugenzi wa Programu kutoka
Taasisi ya Uchumi na Utafiti wa Kijamii nchini (ESRF) Dkt Tausi Kida
akitoa mada juu ya umuhimu wa kutafuta rasilimali za kutosha katika
kufikia malengo ya milenia hasa kwa nchini zinazoendelea.
Balozi Mushy aliongeza kwamba
serikali ya Tanzania imeweka msimamo huo zaidi hivi karibuni na Rais
Jakaya Kikwete aliagiza hivyo kwa maofisa wa Wizara ya Mambo ya Nje
pamoja na Waziri husika kukataa shinikizo la kukubali swala ushoga kama
agenda za maendeleo.
Amesema kwamba watanzania wanataka
maswala yanayowagusa kama vile maji, elimu, huduma bora za afya,
miundombinu ya umeme, ajira, umaskini na kuondoa umaskini wa kipato.
Balozi Mushy alifafanua zaidi kwamba
mambo ya ushoga na ndoa za jinsia yanakwenda kinyume na maadili ya
watanzania, maisha, historia, utamaduni, mila na desturi za mtanzania
sinakataza maswala ya ushoga.
Amesema kwamba serikali inatambua
kwamba sheria ya mwenendo wa makosa ya kujamiiana yaliwekwa na mkoloni
mwingereza kabla ya uhuru na serikali ya Tanganyika imerithi kutoka
kwenye serikali ya mwingereza.
Mkurugenzi wa Idara Ushirikiano
wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy akizungumza kwenye warsha ya siku
moja kuhusu Malengo ya Milenia kwa washiriki mbalimbali na kwa kiasi
ngani Tanzania imeweza kufikia malengo hayo.
“Watanzania na Afrika kwa ujumla
inataka malengo ya millennia na haki za binadamu zizifike mahali
kuwadharirisha watu kutoka bara hili kwa kuruhusu mambo yanayokwenda
kinyume na historia yao, mila na desturi za mwafrika,”aliongeza.
Kwa upande wake, Mhadhiri kutoka
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt Osward Mashindano amesema kwamba
malengo ya milenia kwa kiasi kikubwa yamefikiwa na Tanzania hasa katika
upande wa elimu na kupunguza vifo vya wakinamama na watoto wakati wa
kujifungua.
“leo tumekutana hapa kuzungumza ni
kwa kiasi ngani nchi yetu ya Tanzania imefikia malengo ya milenia na
changamoto ni zipi katika malengo mapya ambayo ni 17 badala ya 8 ya
awali,” aliongeza
Dkt Mashindano alifafanua kwamba ni
lazima sasa serikali kutazama katika Nyanja za ubora katika huduma hizi
muhimu kwa jamii baada ya kufikia lengo la kuandikisha watoto wenye umri
wa kwenda shule kwa asilimia 85.
Mhadhiri wa kutoka Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam, Dkt Osward Mashindano akifafanua umuhimu wa
kuwashirikisha wananchi wa ngazi ya chini kuhusu maswala ya malengo ya
milenia ili yaweze kufikiwa kwa urahisi zaidi.
Aliongeza kwamba Tanzania na dunia
kwa ujumla wameona ni muhimu kuweka agenda ya ubora katika kila agenda
za malengo ya milenia kwa nchi zote ambao ni wanachama wa Umoja wa
Mataifa.
Dkt Tausi Kida, Mkurugenzi wa
Programu wa Taasisi ya Uchumi na Utafiti wa Kijamii, amesema kwamba
malengo haya ya milenia ni lazima yaguse maisha ya watu katika ngazi ya
chini ili matokeo chanya yaweze kuonekana kwenye jamii
Amesema kwamba ni lazima nchi
zilizoendelea ziweke mkazo katika kuhakikisha kwamba nchini
zinazoendelea zinajengewa uwezo wa kutafuta fedha za kutimiza malengo ya
milenia.
Mdau akichangia mada yake.
Wadau wakifurahia jambo wakati ya warsha hiyo.
Wadau mbalimbali walioudhuria wakifuatilia mada mbalimbali.
CREADIT:MAGANGAONE
Post a Comment