0


  
Mwaandishi wetu  Liwale….

Wakulima wa kijiji cha kimambi wilaya ya Liwale mkoani Lindi wameiomba serikali kuingilia kati mgogoro uliozuka kati ya wakulima na wafugaji baada yafugaji kuendesha shughuli za malisho kwenye maeneo ya wakulima na kusababisha uharibifu wa mazao.
 
Akizungumza kwa niaba ya wakulima wa kijiji hicho Dalali Makanjila alisema wakulima zaidi ya 120 wa vitogoji vya Tandawala wamevamiwa na wafugaji ambao wametengewa eneo maaalumu la kuendeshea shughuli zao zan ufugaji,
Makanjila alisema mgogoro usipotafutiwa ufumbuzi mapema unaweza kuleta madhara makubwa ,hivyo ni mkuu wa wilaya tu ambaye anaweza kutatua tatizo kutokana na watendaji na viongozi wa kijiji  kuwaunga mkono wafugaji hao,
‘’Mkuu wa wilaya anatakiwa kufika kabla ya mambo hayajawa makubwa endapo ataendelea kuchelewa  hasira za wakulima zinaweza kuwa kali dhidi ya mifungo na kusababisha vurugu’’alisema Makanjila
Sharifa Kigogo alisema pamoja na kupeleka malalamiko yao kwa viongozi wa kijiji bado kunaonekana kuna jambo la kuwalinda  wafugaji hao hali ambayo inawatia hofu wakulima kuwa kuna mchezo mchafuunachezwa na viongozi wa serikali ya kijiji.
Kigogo alisema wananchi wanaitaka serikali ifanye haraka kuhitisha mkutano baina ya wakulima na wafugaji ili kuwarejesha wafugaji eneo walilopangiwa  la kuendesha shughuli zao za mifugo.
Kwa upande wa mkuu wa wilaya Liwale Amphrey Mmbaga alisema tatizo la wafugaji kuingia kwenye  mashamba ya wakulima analitambua  na ofisi yake imeanza kulifanyia kazi ,baada ya kubaini kuwa chanzo cha mgogoro huyo ni viongozi wa serikali ya kijiji hicho.chanzo sauti ya kusini

Post a Comment

 
Top