Wanafunzi wa shule za msingi za Namihu na Nangando wilayani Liwale mkoani Lindi wanalazimika kujisaidia vichakani kutokana na shule hizo kukosa vyoo kwa muda mrefu sasa.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti wanafunzi wa shule hizo walisema kuwa tatizo hilo
limekuwa kero kwa waanfunzi kwani wakati mwingine ulazimika kukatisha
masomo kutafuta mahali pa kujisaidia ikiweo mikoroshoni.
Musa
mohamedi mwanafunzi wa shule ya msingi Namihu alisema shule yao ina
wanafunzi zaidi ya 200 na walimu 8 lakini hawana vyoo hali ambayo
imekuwa kero kwa wanafunzi na walimu wa shule hiyo.
Mohamedi
alisema mbali na tatizo la vyoo pia shule inakabiliwa na upungufu wa
madarasa hali inayosababisha wanafunzi wa darasa la kwanza hadi la tatu
kusoma kwa awamu ya asubuhi na mchana.
Nae
Fatuma Badi mwanafunzi wa shule ya Nangando alisema kuwa shule yao
inawanafunzi zaidi 300 lakini hawana vyoo vya uhakika hali ambayo
inaweza kuwasabishia kupatwa na maradhi na magongwa ya kuambukizi
ikiwemo kuhara na kuhara damu.
Kwa
upande wake diwani wa kata ya Mbaya Ali Kiyoi alisema kuwa halmashauri
imetenga fedha kwa ajili ya kutekeleza ujenzi wa vyoo matundu manane
kwa ajili ya wanafunzi na mawili kwa ajili ya walimu.
Kiyoi
aliongeza kuwa hatua mbalimbali zinachukuliwa ili wanafunzi waweze
kusoma katika mazingira mazuri ikiwemo pamoja na kuwashawishi wazazi
kushiriki kuchangia maendeleo ya elimu ikiwemo ujenzi wa miundombinu wa
shule.CHANZO:SAUTI YA KUSINI
Post a Comment