0

Mataifa wahisani wamechelewesha msaada wa kuipiga jeki bajeti ya Tanzania hadi pale uchunguzi kuhusu madai ya ufisadi katika sekta ya nishati utakapotolewa na hatua muafaka kuchukuliwa. Kundi la wahisani hao linalojumuisha Finland, Ujerumani, Uingereza, Norway, Sweden, Denmark, Kamisheni ya Umoja wa Ulaya, Ireland, Canada, Japan, Benki ya Dunia na Benki ya Maendeleo ya Afrika, hadi sasa wametoa kiasi cha dola milioni 69 kama sehemu ya ahadi ya msaada wa dola milioni 558 kukidhi mahitaji katika bajeti ya Tanzania.DW

Post a Comment

 
Top